Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro akisikiliza kero za wananchi na migogoro
ambapo zaidi ya wananchi 200 wamepatiwa huduma.
Na Mwandishi wetu Richard Bagolele ,Picha na Stella Herman.
Mamia ya wananchi wa Wilaya ya Shinyanga leo wamejitokeza kwa wingi kuwasilisha kero zao katika Kliniki ya utatuzi wa kero zawananchi iliyoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe.Wakili Julius Mtatiro kwa lengo la kutatua kero hizo.
Akifungua Kliniki hiyo,Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe.Wakili Julius Mtatiro amesema kupitia Kliniki hiyo wamejipanga Kusikiliza na kutatua kero hizo kupitia timu tano za wataalamu kutoka Halmashauri za Wilaya ya Shinyanga ambapo amesema wananchi wote watasilizwa na kero hizo zitapatiwa ufumbuzi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akitoa salamu zake kupitia simu ya Mkuu wa Wilaya amewapongeza wananchi hao waliojitokeza kuwasilisha kero zao ambapo amesema kupitia Kliniki hiyo lazima kuwe na utatuzi wa haraka wa kero hizo kupitia kwa Mkuu wa Wilaya ya Timu ya wataalamu kutoka Manispaa ya Shinyanga na Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Kwa upande wake afisa ardhi kutoka Manispaa ya Shinyanga Bi. Lela Amos amesema migogoro au kero zitokanazo na ardhi zimekuwa zikisababishwa na wahusika kwenda mahakamani katika hatua za awali za migogoro pasipo kuanzia ofisi ya ardhi ambapo kungekuwa na uwezekano wa kupunguza migogoro hiyo.
Amezitaja sababu zingine ni pamoja na wananchi kutokujua Sheria ya masuala ya ardhi hususani wakati wa mauziano ya viwanja na mashamba hivyo amewaomba wananchi hao waliofika kuwasilisha kero zao kujenga tabia ya kufika ofisi za ardhi mahali husika kabla ya mauziano sambamba na kupata elimu ya masuala mbalimbali yahusuyo ardhi.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika Kliniki hiyo wamempongeza Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Wakili Julius Mtatiro kwa kuanzisha zoezi hilo ambapo amesema kupitia Kliniki hiyo wana imani kero nyingi zitatatuliwa na kupunguza migogoro wilayani Shinyanga.
Katika Kliniki hiyo hiyo ya siku moja mamia ya wananchi waliojitokeza waliwasilisha kero kupitia timu mbalimbali za wataalamu waliofika mahali hapo kwa ajili ya utatuzi wa kero ambapo katika hatua ya kwanza timu hizo zitapokea kero hizo

watumishi wa Halmashauri wakiwa tayari kusikiliza kero na migogoro ya wananchi


Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro akisikiliza kero za wananchi



















0 Comments