6/recent/ticker-posts

MKURUGENZI SALU SECURITY AZINDUZI ALBAM YA MSHINDI WA YOTE ,KWAYA YA NVC NGOKOLO KANISA LA AIC SHINYANGA



Mkurugenzi wa kampuni ya Salu Security Bandora Salum Mirambo akizindua albam ya Mshindi wa yote kwaya ya NgokoloVijana Choir  (NVC) katika kaniasa la AIC Ngokolo Manispaa ya Shinyanga 

NA AMO BLOG SHINYANGA 

Mkurugenzi wa kampuni ya Salu Security Bandora Salum Mirambo leo Jumapili Julai 16,2023 katika Kanisa la AICT Ngokolo Manispaa ya Shinyanga ameongoza uzinduzi wa albam ya Mshindi wa yote kwaya ya NgokoloVijana Choir  (NVC) katika kaniasa la AIC Ngokolo Manispaa ya Shinyanga sambamba na kuchangisha fedha kwa ajili ya kuunga mkono kwa ya hiyo .

Akizungumza na waumini wakanisa la AICT Ngokolo katika uzinduzi huo Bandora  amewashukuru waumini wa Kanisa la AIC Ngokolo Shinyanga kwa kuendelea kumkumbuka na kumshirikisha katika shughuli za kijamii hususani za kanisa huku akinukuu kitabu kitakatifu biblia Mithali 8: 17-21, amemshukuru Mungu kwa neema zake na kwa upendo mkubwa kwa taifa letu.

Bandora amewaomba waumini na wakristo kumuombea mhe Rais Samia Suluhu Hassan, “Tumuombee mama yetu na Rais wetu maisha marefu na afya njema azidi kutuongoza kwa hekima na busara, pia naomba waumini muendelee kuliombea taifa amani, utulivu na upendo".

Pia Bandora amewasii wazazi na walezi kuimalisha malezi ya watoto wao ikiwa ni pamoja na kushirikiana na serikali kukemea vitendo vya ukatili na mmomonyoko wa maadili hali itakayo saidia kuwa na kizazi chenye hofu ya mungu katika jamii huku akiwataka vijana wakanisa hilo kufanya kazi ili kujiletea maendeleo na kuepuka kufanya matendo ya sio faa .

Kwa upande wake Katibu wa kwaya ya NgokoloVijana Choir  (NVC ) Gaspary Elias akisoma risala ya kwaya hiyo mbele ya mgeni Rasmi ameeleza kuwa kwaya hiyo imakabiliwa na changamoto ya ununuzi wa vyombo vya mziki licha ya kwaya hiyo kufanikiwa kizindua Albam yenyenyimbo nane ambazo zitasambazwa katika maeneo mbalimbali ya Shinyanga na nje ya Shinyanga  kwa lengo lakuhubiri na kulitangaza neno la mungu.

Mkurugenzi wa kampuni ya Salu Security Bandora Salum Mirambo akipokea risala.


Burudani zinaendelea.


Mkurugenzi wa kampuni ya Salu Security Bandora Salum Mirambo akijiandaa kuzindua albam ya wimbo wa Mshindi wa yote kwaya ya NgokoloVijana Choir  (NVC) katika kaniasa la AIC Ngokolo Manispaa ya Shinyanga 




Post a Comment

0 Comments