Baadhi ya wahitimu 191 wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto wakiwa katika Mahafali ya 69 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho na ya 14 tangu kipate usajili mpya kwa jina la Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto, yaliyofanyika Julai 24, 2026.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto, Dkt. Joseph Mayala, akihutubia washiriki wa Mahafali ya 69 ya chuo hicho tangu kuanzishwa kwake na ya 14 tangu kipate usajili mpya kama Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto.

Mkuu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto, Paschal Shiluka, akizungumza wakati wa Mahafali ya 69 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho na ya 14 tangu kipate usajili mpya kwa jina la Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto, yaliyofanyika Julai 24, 2026.
Katibu Mkuu wa Kanisa la AICT, Josephales Mtembe, akizungumza wakati wa Mahafali ya 69 tangu kuanzishwa kwa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto na ya 14 tangu kipate usajili mpya kwa jina la Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto, yaliyofanyika Julai 24, 2026.
Jumla ya wahitimu 191 wametunukiwa vyeti vya Astashahada na Shahada katika Mahafali ya 69 ya Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto, huku Baraza la Wadhamini la Kanisa la AICT likiitaka menejimenti ya chuo kuharakisha mchakato wa kukipandisha hadhi kuwa chuo kikuu ili kuongeza uwezo wa udahili na kupanua wigo wa utoaji wa elimu ya afya nchini.
Mahafali hayo ni ya 69 tangu chuo hicho kianzishwe, lakini ni ya 14 tangu kipate usajili mpya kwa jina la Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto. Awali, taasisi hiyo ilisajiliwa na kuendesha shughuli zake kama Chuo cha Uuguzi Kolandoto kabla ya kupanua wigo wa programu za masomo na kupata usajili mpya.
Akizungumza katika mahafali hayo yaliyofanyika Julai 24, 2026, Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la Kanisa la AICT, Dkt. Joseph Mayala, amesema ni wakati muafaka kwa chuo hicho kupandishwa hadhi kuwa chuo kikuu ili kiweze kutoa mchango mkubwa zaidi katika maendeleo ya sekta ya afya nchini.
Amesema hatua hiyo itakiwezesha chuo kuongeza programu za masomo, kupokea wanafunzi wengi zaidi na kuimarisha uwezo wake wa kuzalisha wataalamu wa afya wenye ujuzi na weledi unaohitajika katika soko la ajira.
"Tunataka kuona mchakato wa kukipandisha hadhi chuo hiki unakamilika kwa wakati ili kiweze kuongeza uwezo wake wa kutoa elimu ya juu na kuzalisha wataalamu wengi zaidi watakaohudumia jamii," amesema Dkt. Mayala.
Aidha, amesema Serikali imepanga kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika eneo la Kolandoto, ikiwemo ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka barabara kuu hadi chuoni pamoja na ujenzi wa kituo cha polisi katika mwaka wa fedha 2026/2027.
Kwa mujibu wake, miradi hiyo itakapokamilika itaboresha mazingira ya utoaji wa huduma, kurahisisha usafiri kwa wanafunzi, watumishi na wagonjwa wanaofika Hospitali ya Kolandoto, sambamba na kuimarisha usalama katika eneo hilo.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Kanisa la AICT, Josephat Mtembe, amesema Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto kinaendelea kutekeleza maono ya Kanisa la AICT ya kuwahudumia wananchi kupitia elimu, afya na huduma nyingine za kijamii.
Amesema tangu kuanzishwa kwake, chuo kimepata maendeleo makubwa, ikiwemo kuongezeka kwa programu za masomo kutoka programu moja hadi saba, hatua inayoonesha kukua kwa taasisi hiyo na uwezo wake wa kuandaa wataalamu wa afya wanaokidhi mahitaji ya taifa.
Naye Mkuu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto, Paschal Shiluka, amesema chuo hicho kimeendelea kukua kwa kasi, ambapo idadi ya wanafunzi imeongezeka kutoka wanafunzi 12 wakati wa kuanzishwa hadi kufikia wanafunzi 3,350 kwa sasa.
Amesema ongezeko hilo linaonesha imani kubwa ya jamii katika ubora wa mafunzo yanayotolewa chuoni hapo pamoja na mchango wake katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kuongeza idadi ya wataalamu wa afya nchini.
Shiluka amesema pamoja na mafanikio hayo, chuo bado kinakabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo hitaji la kukamilishwa kwa ujenzi wa kituo cha polisi katika eneo hilo pamoja na uboreshaji wa barabara inayounganisha chuo na Hospitali ya Kolandoto kwa kiwango cha lami.
Ameongeza kuwa menejimenti itaendelea kushirikiana na Serikali, Kanisa la AICT na wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuimarisha miundombinu ya chuo, kuongeza ubora wa mazingira ya kujifunzia na kufundishia, pamoja na kupanua huduma za elimu ya afya zinazotolewa.
Wakati huo huo, wahitimu waliotunukiwa vyeti wamehimizwa kwenda kuitumikia jamii kwa weledi, uadilifu na kuzingatia maadili ya taaluma zao. Pia wamekumbushwa kuepuka vitendo vya rushwa, ukiukwaji wa sheria na mienendo isiyofaa ambayo inaweza kuathiri taaluma na heshima ya kada ya afya.
Mahafali hayo yamekuwa kielelezo cha ukuaji wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto kutoka kilipoanzishwa kama Chuo cha Uuguzi Kolandoto hadi kuwa taasisi inayotoa programu mbalimbali za elimu ya afya. Aidha, yameendelea kuthibitisha mchango wa chuo hicho katika kuzalisha wataalamu wa afya wenye sifa na kuunga mkono jitihada za Serikali za kuboresha huduma za afya nchini.

0 Comments