6/recent/ticker-posts

UBIA WA BARRICK NA TWIGA WAZIDI KUWA KIOO CHA USHIRIKIANO WA SERIKALI NA SEKTA BINAFSI TASNIA YA MADINI

 

Meneja Mkazi wa Barrick nchini, Dk. Melkiory Ngido, akipokea Tuzo ya Rais ya Mlipakodi Kinara kwa niaba ya Barrick Mining Corporation kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, wakati wa hafla ya utoaji wa Tuzo za Rais kwa Walipakodi Wakubwa iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Profesa Riziki Shemdoe akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa awamu ya pili ya mpango wa Barrick–Twiga Future Forward Education Program katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Kibaigwa, mkoani Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Profesa Riziki Shemdoe akisalimia wakazi wa Kibaigwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa awamu ya pili ya mpango wa Barrick–Twiga Future Forward Education Program katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Kibaigwa, mkoani Dodoma. Kushoto ni
Meneja Mkazi wa Barrick nchini, Dkt. Melkiory Ngido.

**

Katika kipindi cha miaka karibia saba iliyopita tangu Serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Twiga kuingia ubia na kampuni ya uchimbaji wa dhahabu ya Barrick Mining Corporation yamepatikana mafanikio makubwa yenye athari Chanya ambayo kadri siku zinavyozidi kusonga mbele na kuwa kioo cha ushirikiano wa serikali na sekta binafsi.

Mafanikio haya yanaenda sambamba na mchango wa taifa katika sekta ya madini katika Pato la Taifa ambao kwa sasa inachangia asilimia 10% ambapo kampuni ya Barrick na Twiga kupitia uendeshaji wa migodi ya Bulyanhulu, North Mara na Buzwagi ambao uko katika mchakato wa kufungwa ina mchango mkubwa katika ukuaji huu wa mchango wa sekta.

Tangu ubia huu uanze karibia miaka saba iliyopita tumeshuhudia ukichangia kulipa kiasi kikubwa cha kodi serikali pia kuongoza katika kutoa magawio, gawio, mrabaha, kufanikisha miradi ya kijamii katika sekta za afya, elimu, maji safi, miundombinu ya barabara, ajira kupitia fedha za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) na kunufaisha wazabuni na wakandarasi wa ndani.
Meneja Mkazi wa Barrick nchini Tanzania, Dk. Melkiory Ngido (kulia), akimkabidhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan (kushoto), hundi mfano (Dummy Cheque). Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Twiga Minerals Corporation, Mathias Chanila.

Katika kipindi cha mwaka huu Barrick-Twiga imeweka rekodi ya mafanikio kwa kutoa gawio kubwa Serikalini kati ya makampuni zaidi ya 300 ambayo serikali ina hisa ambapo imetoa shilingi bilioni 221.9 ambapo ni mwendelezo wa kutoa gawio katika miaka iliyopita mwaka wa fedha 2021/2022 ilitoa bilioni 53.5,mwaka 2022/2023 ilitoa shilingi bilioni 84, na mwaka mwaka 2024/2025 ilitoa kiasi cha shilingi bilioni 93.6.

Mbali na kutoa gawio nono, Barrick-Twiga hivi karibuni ilitangazwa na kutunukiwa tuzo ya Rais ya Mlipa kodi bora katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2024/2025 wakati wa hafla ya siku ya kuwatambua walipa kodi bora nchini iliyoambatana na maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mafanikio haya ya kuwa kinara wa kutoa gawio na kodi mwaka huu yamekuja wakati kampuni ya Barrick hivi karibuni imetoa ripoti ya utekelezaji wa masuala endelevu ya mwaka kipindi cha mwaka uliopita ikibainisha kwa kina utendaji wa shughuli zake katika sehemu mbalimbali duniani na kuweka msisitizo kwa kuendelea kufanya uwekezaji wenye kuleta manufaa kwenye maeneo ya biashara zake.

Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Hill akiongelea ripoti hiyo alisisitiza kuwa kampuni itaendelea kutekeleza sera zake madhubuti ambazo zinaendelea kuleta mafanikio "Tunapoingia katika awamu mpya ya kusisimua ya ukuaji na kupata mafanikio, uendelevu unasalia kuwa msingi wa jinsi tunavyofanya kazi.

Kanuni ambazo zimetuongoza kwa miaka mingi bado hazijabadilika: kuwaweka watu wetu salama, uchimbaji madini kwa uwajibikaji, kujenga ushirikiano imara, na kutoa thamani ya muda mrefu ambayo inashirikiwa na washikadau wetu wote”, alisema.

Ripoti hiyo imebainisha kuwa hadi mwaka jana asilimia 96% ya wafanyakazi wa Barrick sehemu mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania na asilimia 76% ya wazabuni wake walitoka katika nchi mwenyeji ambapo pia kampuni ilitumia zaidi ya dola bilioni USD 7.1 katika matumizi na wasambazaji wa ndani na nchi mwenyeji pia iliwekeza zaidi ya dola milioni USD 62 katika mipango ya maendeleo ya jamii.

Kwa hapa Tanzania uekelezaji wa mkakati huu endelevu unaendelea kufanikisha masuala mbalimbali ambapo tangu ubia wa Barrick na Twiga uanze mwaka 2019,Barrick imewekeza zaidi ya dola bilioni USD 4.79 katika uchumi wa Tanzania kupitia kulipa kodi na tozo mbalimbali, gawio, mrabaha, mishahara, malipo ya wazabuni wa ndani na utekelezaji wa miradi ya kijamii.

Barrick imekuwa ikitekeleza sera ya maudhui ya ndani (Local Content)kwa vitendo ambapo inafanya manunuzi ya bidhaa za uzalishaji asilimia zaidi ya 90 kutoka kwa wazabuni wa ndani na asilimia 96 ya wafanyakazi wake ni watanzania wakiwemo wanaotokea katika maeneo ilipo migodi yake ya North Mara na Bulyanhulu pia viongozi wote wa nafasi za juu katika uendeshaji wa shughuli zake hapa nchini ni Watanzania.

Baadhi ya miradi mikubwa inayotekelezwa na Barrick-Twiga ambayo itaacha alama kwa vijazi vizavyo mojawapo ni mradi wa kusongesha mustakabali wa elimu nchini-‘Barrick-Twiga Future Forward Education Program’ ambao umelenga kuongeza na kuboresha miundombinu ya shule za sekondari za serikali za elimu ya juu (Advanced Level) ili kuongeza idadi ya wanafunzi wanaochaguliwa ambao walikuwa wanakosa fursa ya kuendelea na masomo kutokana na uhaba wa miundombinu sambamba na kuhakikisha wanapata elimu katika mazingira rafiki.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Profesa Riziki Shemdoe akizindua jiwe la msingi la ujenzi wa madarasa sita na mabweni mawili katika Shule ya Sekondari Kibaigwa, mkoani Dodoma. Kushoto ni Meneja wa Fedha wa Barrick nchini, Penina Kituku.

Mradi huu ambao umeingia katika awamu ya pili utagharimu kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 70.5 ukilenga kujenga madarasa 1,090,majengo ya maliwato na vyoo 1,660 na mabweni 270 katika shule 161 nchini kote.

Katika awamu ya kwanza imefanikisha ujenzi wa vyumba vya madarasa vya kisasa 374,mabweni ya kisasa 89 na vyoo 569.
Wakati mradi umeingia awamu ya pili mafanikio yake yameanza kuonekana kupitia matokeo ya kidato cha sita yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) hivi karibuni ambayo imebainisha kuwa jumla ya watahiniwa 124,603 sawa na asilimia 99.56 wamepata ufaulu mzuri wa daraja la kwanza hadi la tatu na kuendeleza rekodi ya mwaka uliotangulia ambapo wanafunzi walisomea katika mazingira mazuri ya miundombinu iliyoboreshwa pia Tume ya Vyuo vikuu nchini (TCU)imebainisha kuwa nafasi ya wanafunzi wa kujiunga na vyuo vikuu nchini kwa masomo ya shahada ya kwanza zimeongezeka kufikia 170,000.

Mradi mwingine wa Barrick utakaoacha alama ni wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami ya Kahama-Bulyanhulu JCT- Kakola yenye kilomita 73 unaotekelezwa na kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation kwa ufadhili wa migodi ya Barrick-Twiga wa gharama ya shilingi bilioni 101.2 ambao ujenzi wake unaendelea.
Mchakato wa kumwaga lami katika barabara ya Kahama-Kakola inayojengwa kwa uwezeshaji wa kampuni ya Barrick nchini ukiendelea.

Barrick-Twiga pia mbali na kuwekeza katika miundombinu pia imejikita kujenga kizazi cha wataalamu wa baadaye wa sekta ya madini ambapo karibuni ilisaini mkataba wa miaka 10 na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo itafadhili kiasi cha shilingi bilioni 25 kwa ajili ya ufadhili wa masomo kwa wanafunzi zaidi ya 500, kuwezesha tafiti, na kutoa mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi wa madini na jiolojia kupitia UDSM School of Mines and Geosciences (SOMG) pia imetoa ufadhili kwa wanafunzi watano watanzania kupata utaalamu wa fani ya madini nchini Afrika ya Kusini.

Mafanikio mengi yaliyopatikana kupitia ubia hii yanadhihirisha kuwa Serikali ikifanya kazi kwa ushirikiano na sekta binafsi taifa letu litaweza kupata maendeleo ya haraka.

Kama kampuni moja imeweza kuleta mafanikio haya inamaanisha tukiwa na makampuni mengi makubwa yanayoendeshwa kwa weredi kama Barrick katika sekta mbalimbali taifa letu linaweza kusonga mbele kimaendeleo haraka.

Post a Comment

0 Comments