6/recent/ticker-posts

MBUNGE JIMBO LA NGARA NDAISABA RUHORO AZINDUA RASMI KAMPUNI YA ULINZI NGARA SECURITY COMPANY LIMITED





Mbunge wa Jimbo la Ngara, Ndaisaba Ruhoro akizindua kumpuni ya ulinzi ya Ngara Security.

Na Mwandishi wetu Amo Blog Ngara

Mbunge wa jimbo la Ngara Ndaisaba George Ruhoro amezindua kampuni ya ulinzi ya Ngara SeCurity Company Limitedi iliyopo katika eneo la Jankisheni Mkabala na Jengo la Halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera.

Uzinduzi wa Kampuni ya Ngara Security Company Limited umefanyika leo Augost ,9,2023 katika eneo La Jankisheni Wilayani Ngara mkoani Kagera ukiongozwa na Mhe.Ndaisaba Ruhoro mbunge wa jimbo la Ngara akiongozana na viongozi mbalimbali wa chama na serikali pamija na wananchi.

Akizindua kampuni hiyo Mhe.Ndaisaba Ruhoro ametoa Shilingi milioni moja pamoja na ajira kwa walinzi wawili wa kampuni hiyo ikiwa nisehemu ya kuunga mkono jitihada zilizo fanywa na  uongozi wa kampuni ya Ngara Security Company Limited 

Aidha Mhe.Ruhoro pamoja na kutoa pongezi kwa uongozi wa Kampuni pia amewa sii wananchi kuendelea kumuombea Rais  Dkt.Samia kwa kazi kubwa anayo ifanya kwa ajili ya kuwaletea wananchi maendeleo ikiwemo kutoa fulsa na kuboresha mazingira ya uwekezaji kwa wananchi.

Naye mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Ngara Security Company Limited John Mpekeye amemshukuru mbunge wa jimbo la Ngara kwa Mhe.Ndaisaba Ruhoro kwa kuzindua kampuni hiyo huku akiwaomba wadau wamaendeleo pamoja na wana nchi wa wilaya ya Ngara kuitumia kampuni hiyo katika Shughuli za ulinzi.

Kwa upande wake Mkurugenzi idara ya Fedha na Mipango Jack Buzoya ameahidi kushirikiana na wananchi katika kuimalisha ulinzi na usalama ,huku akiomba wadau wamaendeleo kumshauri pale kampuni yake inapo kwenda kinyume hali itakayo saidia kuboresha utendaji kazi wa kampuni hiyo.

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Ngara Security Company limited John Mpekeye akimkaribisha mbunge wa jimbo la Ngara kuzindua kampuni hiyo.

Diwani wa kata ya Ngara mjini Kenedy Staford Akizungumza baada ya halfa ya uzinduzi wa kampuni ya ulinzi ya Ngara Security Company Limite
Mbunge wa jimbo la Ngara Ndaisaba Ruhoro akizindua mavazi yatakayo tumiwa na kampuni ya ulinzi wakati wa kutekeleza wajibu wao.

Mbunge wa jimbo la Ngara Ndaisaba Ruhoro akizindua mavazi yatakayo tumiwa na kampuni ya ulinzi wakati wa kutekeleza wajibu wao.

Mbunge wa jimbo la Ngara Ndaisaba Ruhoro akizindua mavazi yatakayo tumiwa na kampuni ya ulinzi wakati wa kutekeleza wajibu wao.

Mbunge wa jimbo la Ngara Ndaisaba Ruhoro akizungu mza na wananchi walio shiriki hafla ya  uzinduzi wa kampuni ya ulinzi ya Ngara Security Company Limited .

Post a Comment

0 Comments