6/recent/ticker-posts

BARRICK YAWEZESHA WANAFUNZI VYUO VIKUU KILIMANJARO KUPATIWA UTAMBUZI WA FURSA KUPITIA KONGAMANO LA AIESEC 2026

  

Meneja uzalishaji (Plant Manager wa Barrick Bulyanhulu), Raymond Zakayo akiongea na Wanafunzi katika kongamano hilo
Meneja uzalishaji (Plant Manager wa Barrick Bulyanhulu), Raymond Zakayo akiongea na Wanafunzi katika kongamano hilo
Baadhi ya wafanyakazi wa Barrick walioshiriki kongamano hilo katika picha ya pamoja
Watoa mada kutoka taasisi mbalimbali katika picha ya pamoja na viongozi wa AISEC

****

Wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani Kilimanjaro wamepata fursa ya kupata elimu ya kuchangamkia fursa za kupata mafanikio kupitia elimu yao katika kongamano lililoandaliwa na taasisi ya AIESEC.

Katika kongamano hilo la aina yake, lililofanyika katika Chuo cha Ushirika Moshi kwa udhamini wa kampuni ya Barrick nchini, wanafunzi waliweza kujua kwa undani shughuli za Barrick nchini na makampuni mbalimbali makubwa ya kibiashara na jinsi ya kutafuta fursa ya kujiunga nayo pindi wamalizapo masomo yao ya elimu ya juu.

Wanafunzi pia walijengewa uwezo kutoka kwa wafanyakazi wa Barrick na taasisi nyinginezo kuhusiana na jinsi ya kuchangamkia fursa zinazojitokeza,kujiamini,ubunifu na jinsi ya kujiajiiri na kutengeneza fursa za ajira hususani katika kipindi hiki ambacho kuna mabadiliko ya kasi ya matumizi ya sayansi na teknolojia za kisasa duniani kote ambayo yanagusa kila tasnia.

Post a Comment

0 Comments