6/recent/ticker-posts

KATUNDA FC YAENDELEZA UBABE MASHINDANO YA KATAMBI UNDER 17 CUP HATUA YA NUSU FAINALI NA KUTINGA FAINALI

Na Mwandishi wetu Amoj Media Shinyanga.

Mashindano ya mpira wa miguu yanayojulikana kama SHIDIFA Under 17 League, maarufu kama Katambi Under 17 Cup 2025, yameendelea kutimua vumbi katika uwanja wa Sabasaba ikiwa ni hatua ya nusu fainali kwa kuzikutanisha timu ya Katunda Fc dhidi ya timu ya Kambarage Market FC ambapo mpambano huo umemalizika kwa timu ya Katunda Fc kuibuka kidedea kwa kuifunga timu ya Kambarage Makert Mabao manne kwa moja na kupata tiketi ya kutinga fainali.

Mashindano hayo yaliyo anza kutimua vumbi Februari 14, 2025,yakishirikisha timu 16 yanaendelea katika hatua ya nusu fainali kwa udhamini wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Mhe. Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).

Mashindano haya, ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya michezo kwa vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 17, yanatarajiwa kuwa jukwaa la kuibua vipaji vya vijana wa mtaani na wanafunzi wa shule za sekondari katika Manispaa ya Shinyanga.

Katika mashindano hayo Mhe.Katambi ametoa fedha kiasi cha shilingi milioni 6,610,000/- kwa Kamati tendaji ya Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Shinyanga (SHIDIFA) ikiongozwa na mwenyekiti wake Joseph Assey ikiwa ni dhamira  ya dhati ya Mbunge huyo kusaidia maendeleo ya michezo katika jimbo la Shinyanga mjini.

Akizungumza na wanamichezo pamoja na mamia ya mashabiki walio fika uwanjani kutazama mpambano huo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Anord Makombe amemlongeza Mhe.Katambi kwa kujitoa kudhamini ligi hiyo ambayo imechangia kuinua vipaji vya vijana katuka jimbo hilo.

Kwa upande wake katibu wa Mhe.Katambi Bw.Samweli Jackson amesema kuwa fainali itachezwa April 4 na kuziomba timu zilizo fuzu kujiandaa vizuri kwani mgeni rasmi katika fainali hiyo atakuwa Mhe.Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi ambaye pia atakabidhi zawadi mbaimbali kwa washindi walio ibuka kidedea katika mashindano.












Post a Comment

0 Comments