.jpeg)

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi akiwa na viongozi wengine kwenye picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa kampeni ya "Tuwaambie kabla hawajaharibiwa awamu ya pili.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga leo Septemba 29,2025 limezindua rasmi Kimkoa Kampeni ya Tuwaam bie mapema kabla hawajaharibiwa katika Wilaya ya kipolisi Ushetu ,kwa lengo la kuwalinda watoto kutimiza ndoto zao.
Akizindua Kampeni hiyo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga Kamishina msaidizi mwandamizi i(SACP) Janeth Magomi amesema huo ni mpango mahususi unaosimamiwa na kitengo cha Dawati la jinsia na watoto ili kuongeza uelewa kwa Jamii.
Amesema kampeni hiyo inalenga kujenga Jamii yenye misingi ya heshima,usalama na ulinzi wa mtoto kwa kuwawezesha kutimiza ndoto zao na siyo kujiunga na makundia ambayo hayana tija na yanaweza kuwaharibia mwelekeo.



Amesema lengo la kampeni hiyo kuyawezesha makundi hayo yanakuwa salama dhidi ya vitendo vya ukatili pia kuwajenga kuwa wazalendo kwa kutoa elimu dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Amesema wamelenga kuondoa au kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia na kuielimisha jammii kutambua kuwa vitendo vya udhalilishaji ni kosa la jinai na kuripoti ili kuchukuwa hatua za kisheria.
.jpeg)
TAZAMA PICHA ZA ZOEZI LA UZINDUZI WA KAMPENI HIYO HAPA



.jpeg)
.jpeg)


.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)


.jpeg)
.jpeg)
0 Comments