Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake UWT mkoa wa Shinyanga Grace Bizulu akizungumza na wajumbe wa baraza la UWT Mkoa .
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake UWT mkoa wa Shinyanga Grace Bizulu amewataka wanachama wa UWT kishikamana ili kukijenga chama kuliko kuendelea kutendengeneza makundi na kupiga majungu hali ambayo inaweza kukigawa chama hicho na kusababisha mpasuko mkubwa ndani ya jumuiya na CCM.
Grace amesema hayo wakati akizungumza na wajumbe
wa baraza la UWT Mkoa wa Shinyanga, lililofanyika katika ukumbi mdogo wa CCM
mkoa, ambapo amesema kuna baadhi ya watu wamekuwa wakitengeneza makundi na kuwasema viongozi waliopewa dhamana ya kukiongoza chama hicho , hali ambayo imekuwa ikisababisha mpasuko mkubwa kwa wabunge
na wanachama.
Grace amesema kuwa uchaguzi umeisha, kila mmoja afanye
majukumu yake ya kazi haitakiwi tena kupigana mikumbo, ifikie sehemu kila mmoja
ampende mwenzake na kuweza kukisemea vizuri chama cha mapinduzi na kusikiliza
kero zilizopo kwenye jamii na kuzitatua kwa sababu wote ni watoto wa mama mmoja
CCM na tunasimamia ilani ya Chama.
"Imefikia wakati tunaanza kurekodiana mmezidi
hiyo tabia niwaombe muache mara moja, nikimjua mtu anayechonanisha nitamwambia
katibu asimualikie kwenye vikao vyangu, tuweni na hofu ya Mungu tupendane pale
tunapokosea tuambizane tusiendekeze majungu hayajengi yanabomoa,"amesema
Mwenyekiti Bizulu.
"Niwaombe ndugu zangu tuwe na upendo na
mshikamano tusiwe wabomoaji wanaopenda kuvuruga na kujipendekeza, kwani watu
wanaofanya hivyo wanatuharibia mkoa wetu na kuonekana hatuna ushirikiano na
umoja, ndiyo maana tunashindwa kupata wageni wakubwa kwa sababu ya watu
wachache wanaopenda kujipendekeza, amesema Bizulu.
"Sisi kina mama tunatakiwa tuwe na upendo na
mshikamano,tufanye kazi kama tulivyoahidi wakati tunaomba kura kwa wananchi,
niombe huu wakati mniache nifanye kazi, kwa kushirikiana na wabunge wangu wote,
sitaki mambo ya ubaguzi tusibaguane kwamba huyu ni wa nani na huyu ni wanani
tufanye kazi kwa pamoja, wale waomba fedha watafute njia zingine za kushawishi
sio kusema uongo," ameongeza Bizulu.
Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Shinyanga Rucy Mayenga amewaomba wanawake kutoa ushirikiano ili kuhakikisha wanajenga nyumba
ya katibu wa UWT na ofisi ya wabunge kwani wabunge hawapo nyuma katika kufanya
maendeleo ambapo amechangia shilingi milioni 10 kwa ajili ya kujenga nyumba hiyo huku Santiel Kilumba akichangia shilingi milioni 6 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hiyo..
Kwa upande wake Katibu wa UWT mkoa wa Shinyanga Asha Kitandala akiwa na wajumbe wa baraza wametembelea eneo la ujenzi na kukagua ujenzi wa nyumba ya katibu wa UWT
mkoa inayojengwa katika maeneo ya Bushushu kata ya Lubaga ambapo ameeleza kuwa tayari wameanza
ujenzi ambao utachukua siku 16 kufikia tarehe 12, 8, 2023 , ambapo pia katika eneo hilo watajenga vibanda nane kwa
ajili ya biashara.
Kwa upande wake mjumbe wa baraza la UWT Taifa
Christina Gule amewaomba wanawake kuendelea kuwa na ushirikiano ili waweze
kufanya mambo makubwa ndani ya CCM waendelee kutatua kero mbalimbali,
wakishirikiana na wabunge,katika kuinua maendeleo ya jumuiya na chama.
"Wabunge
wetu tunawapenda sana karibuni sana mjisikie vizuri kinachotakiwa ni kuwa na
ushirikiano, sasa mkoa wetu umetulia tuendelee kumuomba Mungu aendelee kutusimamia
ili tuweze kufanya mambo makubwa ndani ya CCM, tuendelee kutatua kero
mbalimbali wabunge wetu njooni tufanye kazi ya UWT kina mama tupo kwa ajili ya
kufanya kazi,amesema Gule
"Ni heshima kubwa kuanzisha ujenzi huu, kwani toka ianzishwe UWT mkoa wa
Shinyanga haijawahi kujengwa nyumba ya katibu wa UWT, na sasa tunaendelea
kujenga tunawashukuru chama mkoa kwa kuendelea kutusapoti na tunawashukuru
wabunge wetu kwa kuendele kutushika mkono tumeanza leo kujenga, niwaombe
wajumbe wa baraza tuendelee kutafuta fedha ili nyumba hii imalizike kwa
wakati,"amesema Gule.
Kikao cha baraza la UWT Mkoa wa Shinyanga
kimefanyika leo katika ukumbi mdogo wa CCM Mkoa, ambapo pia wajumbe wa baraza
hilo waliambatana na mbunge viti maalumu Santel Kilumba kwa ajili ya kukagua
mradi wa ujenzi wa nyumba ya katibu katika maeneo ya Bushushu manispaa ya
Shinyanga.
Mbunge viti maalumu Mkoa wa Shinyanga Lucy Mayenga akizungumza kwenye baraza la UWT Mkoa wa Shinyanga nakuahidi kutoa shilingi milioni 10 kwa ajili ya ujenzi wanyumba ya katibu wa UWT mkoa.
Mbunge viti maalumu Mkoa wa Shinyanga Santiel Kilumba akizungumza kwenye baraza la UWT Mkoa wa Shinyanga na kuahidi kuchangia shilingi milioni 6 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya katibu wa UWT.
Mbunge viti maalumu Mkoa wa Shinyanga Santiel Kilumba akizungumza kwenye baraza la UWT Mkoa wa Shinyanga .
Katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga Sharifa Hassan Mdee akizungumza kwenye kikao cha baraza mkoa wa Shinyanga
0 Comments