
Na Amos John Amo Blog Shinyanga
Leo tarehe 27 Februari 2026, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Ndugu Wallace Karia, akiwa ameambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Azan Logistics, Ndugu Azan Muft, wamefanya ziara maalum katika ofisi za Jambo & Sons Traders Company Limited zilizopo Kahama ikiwani nisehemu ya kutembelea na kukutana na wadau wamichezo walioko mkoani Shinyanga.
Ujumbe huo umepokelewa rasmi na wenyeji wao,Ndugu Gabriel Masanja (GM) pamoja na Ndugu Mohamed Kapufi, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Biashara na Masoko katika ofisi za Jambo & Sons Traders Company Limited zilizopo Manispaa ya Kahama .
Ziara hiyo imelenga kuimarisha mahusiano ya kikazi na kibiashara, pamoja na kujadili fursa za ushirikiano zitakazochochea maendeleo ya michezo na sekta ya biashara kwa ujumla katika mkoa wa Shinyanga na taifa kwa ujumla.
Aidha hatua hiyo inaonesha dhamira ya dhati ya viongozi hao katika kujenga ushirikiano imara kati ya sekta ya michezo na sekta binafsi, kwa lengo la kuleta maendeleo endelevu na yenye tija kwa jamii.
0 Comments