6/recent/ticker-posts

SHANGWE ZA TAWALA AHMED SALUM NA AZZA WAKIREJESHA FOMU MBIO ZA UBUNGE JIMBO LA SOLWA NA ITWANGI


Chanzo - Malunde 1 blog

Wagombea Ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Wilaya ya Shinyanga Vijijini wamerudisha rasmi fomu za kugombea nafasi za Ubunge, tukio lililojaa mshikamano na ishara ya maandalizi makini kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Miongoni mwa wagombea hao ni Ndugu Ahmed Ally Salum, anayewania Ubunge wa Jimbo la Solwa, pamoja na Ndugu Azza Hillal Hamad, mgombea wa Jimbo jipya la Itwangi, ambalo limeundwa baada ya kugawanywa kwa Solwa.

Wote wamerudisha fomu hizo Leo, tarehe 27 Agosti 2025 katika Ofisi za Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) mbele ya viongozi na wanachama wa CCM kutoka Wilaya ya Shinyanga Vijijini.

Wakati wa urejeshaji wa fomu, viongozi wa chama na wafuasi waliowasindikiza wagombea hao wamesisitiza mshikamano wa chama na kuahidi kushirikiana kuhakikisha ushindi wa kishindo kwa tiketi ya CCM.

Viongozi waliokuwepo wamesema hatua hii ni ishara tosha ya mshikamo ndani ya chama na kudhihirisha maandalizi makubwa kuelekea ushindi katika majimbo yote mawili ya Wilaya ya Shinyanga Vijijini, Solwa na Itwangi.
“Leo tunaonesha mshikamano wa CCM; Jimbo la Solwa linaendelea kuwa ngome, na Itwangi linaanza safari yake ya kisiasa yenye matumaini makubwa kwa wananchi wake,” amesema mmoja wa viongozi wa chama





Post a Comment

0 Comments