6/recent/ticker-posts

TIMU MPYA YA BEDUI FC YAIBUKA NA NDOTO ZA KUCHEZA LIGI KUU, YAJIPIMA NGUVU NA SHY TOWN VETERAN SHINYANGA

Timu mpya ya Bedui FC,ambayo imeanza safari yake kwa kujipima nguvu katika mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Shy Town Veteran. 

Na Mwandishi wetu Amoj Media Blog

Soka la mkoa wa Shinyanga limepata msukumo mpya baada ya kuibuka kwa timu mpya ya Bedui FC, ambayo imeanza safari yake kwa kujipima nguvu katika mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Shy Town Veteran mchezo ulio pigwa katika uwanja wa polisi Shinyanga.

Timu hiyo mpya imeanzishwa ikiwa na lengo la kuinua vipaji vya wachezaji wa ndani pamoja na kuongeza ushindani katika soka la mkoa huo.

Mchezo huo wa kirafiki umevutia wadau mbalimbali wa michezo waliojitokeza kushuhudia mwanzo wa safari ya timu hiyo iliyo ibuliwa ndani ya Manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza kuhusu malengo ya timu hiyo, Afisa Habari wa timu Bedui FC, Frenk Mpuya, amesema kuwa ndoto kubwa ya klabu hiyo ni kufika mbali zaidi katika soka la Tanzania, ikiwemo kucheza ligikuu ligi kuu ya Tanzania siku za usoni.

“Lengo letu kubwa ni kujenga timu imara ambayo siku moja itaweza kushiriki ligi kuu. Tunataka kuwapa nafasi vijana wenye vipaji hapa Shinyanga na maeneo mengine kuonyesha uwezo wao,” amesema Mpuya.

Kwa upande wake, msemaji wa timu ya Shy Town Veteran, Self Wamkote, ameipongeza timu ya Bedui FC kwa hatua ya kuanzisha timu ambayo itaongeza chachu ya maendeleo ya soka katika mkoa huo.

Wamkote amesema hatua hiyo ni ya kuungwa mkono na wadau wote wa michezo, huku akitoa ushauri kwa viongozi wa timu hiyo kujikita zaidi katika maandalizi na mazoezi.

“Tunawapongeza kwa kuanzisha timu. Ushauri wetu ni wajikite sana kwenye mazoezi na kucheza michezo mingi ya kirafiki ili wachezaji wao wapate uzoefu na kuimarika zaidi,” amesema Wamkote.

Kuanzishwa kwa timu ya Bedui FC kunatajwa kuwa ni hatua muhimu katika kukuza vipaji vya vijana na kuongeza ushindani wa soka katika mkoa wa Shinyanga, huku wadau wa michezo wakiamini kuwa timu hiyo inaweza kuwa chachu ya maendeleo ya mchezo huo endapo itaendelea kujengwa kwa misingi imara.Timu mpya ya Bedui FC,ambayo imeanza safari yake kwa kujipima nguvu katika mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Shy Town Veteran. Timu ya Shy Town Veteran iliyo cheza mchezo wa kirafiki na timu ya Bedui FC na kuibuka na ushindi. 


Post a Comment

0 Comments