Na Amos John Amoj Media.
Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania (Tiseza), imeanza kampeni ya kitaifa ya kuhamasisha uwekezaji wa ndani, ikilenga kuwajengea Watanzania uelewa na kuondoa dhana kuwa uwekezaji ni kwa wageni pekee, sambamba na kukagua maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kongani za viwanda nchini.
Katika ziara hiyo Meneja uhamasishaji wa uwekezaji wa Ndani Felix John amewasihi watanzania kuendelea kutumia fursa za uwekezaji zilizizopo nchini sambamba na kusajili miradi yao kwenye mamlaka ya uwekezaji na maeneo maalumu ya kiuchumi (TISEZA) hatua itakayowawezesha kukua, kupata tija ya kiuchumi na kupata nafuu ya msamaha wa kodi kwa bidhaa ambazo zinatumika kwenye miradi iliyosajiliwa.
Aidha Felix
ameongeza kuwa kampeni ya kitaifa ya uhamasishaji uwekezaji wa ndani ni sehemu
ya utekelezaji kwa vitendo Mpango wa Taifa wa Maendeleo kwa miaka mitano (FYDP)
inayolenga kutekeleza azma ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kufungua nchi
kwa kuhamasisha uwekezaji.
“Serikali
inaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji kwa kuboresha miundombinu
muhimu kama maji, umeme, barabara na mawasiliano katika maeneo yote ya
uwekezaji,” amesema John.
Naye Mkuu wa
Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita akizungumza mapema na uongozi wa TISEZA ofsini
kwake amepongeza uwepo wa ziara hiyo inayolenga kupita mikoa mbalimbali nchini
ili kujenga uelewa na kueleza kuwa hatua hiyo itasaidia kuamsha ari ya wananchi
kujisajili.
Mboni Mhita,amesema mkoa huo umetenga maeneo mawili makubwa kwa ajili ya uwekezaji wa kiuchumi ambayo ni Buzwagi na Nyanshimbi.
“Hakuna eneo la uwekezaji katika mkoa wa Shinyanga lisilo na miundombinu ya uwezeshaji. Aidha, uwepo wa bandari kavu utaongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi wa mkoa huu,” amesema Mhita.
Kwa upande wake,mwalimu mkuu wa Shule ya Savana Plains Wema Kanyika,amesema kuwa uwekezaji uliofanyika shuleni katika Shule hiyo unanufaisha wanafunzi 936 kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha sita.
“Shule imejengwa katika eneo la hekta 80, ikiwa na wanafunzi 512 wa elimu ya awali na msingi pamoja na wanafunzi 424 wa sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita. Pia tuna wafanyakazi 50 wanaoishi ndani ya shule,” amesema Wema.
Ameongeza
kuwa shule hiyo pia imewekeza katika ufugaji wa ng’ombe kwa ajili ya nyama na
maziwa ya wanafunzi, visima vya maji pamoja na upandaji wa miti ya matunda.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita akizungumza mapema na uongozi wa TISEZA ofsini kwake.
Ungozi wa TISEZA ukiwa ofisini kwa mkuu wa mkoa.

0 Comments