Askofu Magwesela amesema hayo leo Octoba
26,2023 wakati akifungua kikao cha baraza la utendaji la sinodi kuu ya
AICT Dayosisi ya Shinyanga kikao kilicho fanyika kwa lengo la kujadili
changamoto na mafanikio ya dayosisi hiyo.
Askofu Magwesela amesema jitihada zilizo fanywa na waumini wa kanisa
la Africa
Inland Church Tanzania (AICT) zinapaswa kupongezwa maana
jitihada hizo zilifanikisha kurejeshwa kwa Shule ya
Sekondari ya Askofu Nkola (Bishop Nkola Secondary School) iliyokuwa imeuzwa na
hivyo kuleta aibu kubwa kwa kanisa.
Askofu
Magwesela ameeleza kuwa shule hiyo ya kanisa iliuzwa kwa njia ya Mnada mnamo
Februari 23, 2017 baada ya Dayosisi ya Shinyanga kushindwa kurejesha CRDB mkopo
wa kiasi cha TZS 400,000,000.00 (Milioni Mia Nne) ambao shule hiyo iliwekwa
kama dhamana.
Aidha Askofu Magwesela licha ya kuwapongeza waumini wa kanisa la AICT Tanzania pia amewaomba waumini kujitoa kuchangia ujenzi wa nyumba ya Askofu ambayo ujenzi wake umesimama kwa sasa kutokana na kukosekana kwa fedha ya kuendeleza ujenzi huo.
Naye katibu wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania(AICT) Mchungaji Josephales Mtebe ameeleza kuwa ili kudhibiti upotevu wa fedha na mali za kanisa wameajili wakaguzi wa takao fanya ukaguzi katika dayosisi zote za Kanisa hilo ili kubaini wabadhilifu wa fedha na mali za kanisa ndani ya kanisa la AICT.
Kwa upande wake Askofu wa kanisa la Africa
Inland Church Tanzania(AICT) Dayosisi
ya Shinyanga Askofu Zakayo Bugota amewaomba wajumbe wasinodi kuendelea
kuhamasisha maendeleo ya Dayosisi hyo hali itakayo saidia kutimiza malengo na
mipango waliyojiwekea katika kuchochea maendelea ya kanisa la Africa
Inland Church Tanzania(AICT)
Askofu wa kanisa la Africa Inland Church Tanzania(AICT) Dayosisi ya Shinyanga Askofu Zakayo Bugota akimkaribisha kwa maombi askofu mkuu kwa ajili ya ufunguzi wa kikao cha sinodi.
Katibu wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania(AICT) Mchungaji Josephales Mtebe akizungumza na wajumbe wa sinodi .
Katibu wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania(AICT) Mchungaji Josephales Mtebe akizungumza na wajumbe wa sinodi .
Askofu wa kanisa la Africa Inland Church Tanzania(AICT) Dayosisi ya Shinyanga Askofu Zakayo Bugota akiteta jambo na katibu msaidizi wa Dayosisi ya Shinyanga Nuhu Manoni
Askofu wa kanisa la Africa Inland Church Tanzania(AICT) Dayosisi ya Shinyanga Askofu Zakayo Bugota akiteta jambo na katibu msaidizi wa Dayosisi ya Shinyanga Nuhu Manoni
0 Comments