6/recent/ticker-posts

KATIBU WA NEC IDARA YA ORGANAIZESHENI ISSA GAVU ABISHA HODI NA KUZUNGUMZA NA WAZEE SHINYANGA

 Katibu wa NEC Idara ya Organaizesheni Ndg. Issa Gavu akihutubia Baraza la wazee Mkoa wa Shinyanga .

 Na Amo Blog Shinyanga.

 Katibu wa NEC Idara ya Organaizesheni Ndg. Issa Gavu amehutubia Baraza la wazee Mkoa wa Shinyanga na kuwakumbusha wajibu wao kama Baraza la wazee wa CCM ni kushauri na kutengeneza njia sahihi ya ufumbuzi wa Kero na changamoto za wananchi kusudi Chama Cha Mapinduzi kiendelee kushika Atamu pale kinapoingia katika Uchaguzi.

 Hata hivyo Ndg. Issa Gavu amewataka wazee wa Mkoa wa Shinyanga kuendelea kuwakumbusha wanachama kulipa Ada ya uanachama ili watimize haki ya kimsingi ya kuchagua na kuchaguliwa.

 Ndg.Issa Gavu amewataka makatibu wa mikoa na wilaya kusimamia vizuri ufanyikaji wa Vikao katika ngazi husika,msitumie vikao hivyo kwa madhumuni na malengo ya kuwakomoa watu, Vikao viwe ni sehemu ya kutenda Haki, iwe sehemu ya Chemchem ya kupata fikra, mawazo Maoni Ushauri na Mtazamo tukipata nafasi ya kujadiliana tutatoka tukiwa wamoja na kuwapatia ufumbuzi wananchi.

 Aidha baadhi ya wazee wamepata nafasi ya kutoa Ushauri na maoni kwa kusema Wazee wa Shinyanga wanamuunga Mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa Ndg. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuipendelea shinyanga kwa kuhidhinisha fedha nyingi za kuendeleza miradi katika Mkoa wa shinyanga.

 Ndg. Issa Gavu ameshauri wazee kukaa Mkutano wa Baraza la wazee angalau kwa Mwaka Mara mbili ili kujadili na kushauriana namna bora ya kukiendeleza na kukiimarisha Cha Mapinduzi kutambua wapi kilipotoka wapi kilipo na wapi kinatakiwa kwenda, mkifanya hivyo ntakuwa mmekitendea haki Chama Chenu na kuwasaidia vijana kujua namna bora ya kukiongoza na kuwaletea maendeleo wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 Ameyasema hayo leo Tarehe 26 Dec 2023 katika Baraza la wazee Mkoa wa Shinyanga ikiwa ni mwendelezo wa mikoa mingine. 











Post a Comment

0 Comments