6/recent/ticker-posts

WAENDESHA BAJAJI,BODABODA,MAMALISHE NA WAFANYABIASHARA IGUNGA WACHANGAMKIA FURSA YA NMB PESA NA CHAP CHAPU AKkwaAUNTI


Waendesha Bajaji ,Bodaboda ,Mamalishe na Wafanyabiashara wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora wameushukuru na kuupongeza uongozi wa Benki ya NMB kwa kuanzisha Akaunti inayo funguliwa kwa ghalama ya Shilingi 1,000/= Tu  Akaunti Isiyo na Makato ya Mwezi inayotolewa na Benki ya NMB kwa watu wote bila ubaguzi.
 
Wamesema hayo leo Jumamosi Aprili,13 ,2024 katika Mnada wa Igunga Mkoani Tabora wakati wa zoezi la kufungua Akaunti pamoja na kutoa elimu ya umuhimu wa kuwa na Bima ya Faraja ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya kuhamasisha Ufunguaji wa Akaunti kwa watu wote ,Kampeni inayoendeshwa na Uongozi wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi ,NMB Tawi la Igunga kwa kushirikiana na Amos John (Mc Mzungu mweusi )ambaye ni mdau wa benki hiyo.

Aidha wakati wazoezi la kuhamasisha wananchi kufungua akaunti pia wameezwa Fursa ya kwanza inayokuja na akaunti hiyo kuwa pamoja na mteja kuingia moja kwa moja kwenye Huduma Jumuishi za Kifedha kupitia NMB, watoa huduma wake kupatikana maeneo yote ya wananchi ,kuhakikisha kila Mtanzania anakuwa sehemu ya huduma hii inayokuja chini ya kaulimbiu ya ‘Haachwi Mtu".

Pia wananchi wameelezwa kuwa kupitia NMB Pesa mteja anakuwa umeingia moja kwa moja katika huduma ya NMB Mkononi, inayompa wigo mpana wa kujihudumia na kuhudumiwa kibenki bila kwenda matawini au katika ofisi za benki ya NMB ambako unafanya miamala na malipo na manunuzi kidigitali

Hata hivyo kwa wateja walio fungua akaunti ya NMB Pesa akaunti wamepewa elimu juu ya namna mteja wa NMB Pesa anavyo weza kukopa hadi shilingi 500,000 kupitia Mshiko Fasta, huduma ya mikopo isiyohitaji dhamana yoyote wala kujaza fomu. 

#*Tazama picha za mtukio katika mnada wa Igunga leo Aprili 13 ,2024 hapa chini*#




















Post a Comment

0 Comments