6/recent/ticker-posts

KAMPENI YA SELEBRETIKA KIJAMUKAYA YAZINDULIWA RASMI NA KAMPUNI YA JAMBO ,GEORGE AWASHUKURU WATEJA WA BIDHAA ZA JAMUKAYA

Kiongozi Mkuu wa Jambo Media Nickson George, ambaye pia ni kiongozi wa ubunifu na msimamizi wa chapa jambo group akieleza lengo la kuzindua kampeni ya Selebretika KIJAMUKAYA !

 
Kampuni ya jambo group, imezindua kampeni ya Selebretika kijamukaya, kwa kuzalisha vinywaji vikiwa na chapa au Logo maalumu kwa ajili ya msimu wa sikukuu huku wakiaswa wananchi wa mkoa wa Shinyanga na kanda ya ziwa kutumia bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya wazawa (ndani ya nchi) ili kukuza Uchumi wa mkoa wa shinyanga.

Uzinduzi wa kampeni hiyo umefanyika leo Desemba 21,2024 kwenye Ofisi za Jambo Media iliyopo kata ya Ibadakuri Halmashauri ya manispaa ya shinyanga.

Akizindua Kampeni hiyo Kiongozi Mkuu wa Jambo Media Nickson George, ambaye pia ni kiongozi wa ubunifu na msimamizi wa chapa jambo group, amesema, kampeni hiyo ya selebretika kijamukaya, ni kwa ajili ya wateja wao na watumiaji wote wa bidhaa za kampuni hiyo, kufurahia bidhaa za jambo wakiwa na familia zao katika msimu mzima wa sikukuu.

Unawezaje kuiita Sikukuu ikiwa hakuna bidhaa za Jambo hapo mezani? Unawezaje kusema umesherehekea sikukuu kinyumbani ikiwa hujawaalika ndugu na marafiki mfurahie pamoja?,”amesema George.

Aidha 
George, amewaomba wananchi wa kanda ya ziwa au mikoa yote ambayo bidhaa za jambo zinapatikana, na kwamba kama wameshidwa kufika nyumbani kufurahi na familia, watume hata katoni mbili za juice ya jambo dodo, soda, maji na mikate ya jambo, na ambao wanasafiri watumie bidhaa za jambo, ili waselebretike kijamukaya katika msimu huu wa sikukuu.

Sherehekea kinyumbani, Selebretika Kijamukaya na wale uwapendao ukiwa unatumia bidhaa za Jambo,”ameongeza George.

Amesema lengo la kampeni hiyo ni kuona watu wote wanasheherekea sikukuu wakiwa na familia zao, na ambao watashindwa kujumuika kutokana na majukumu, basi wawapigie simu na kuwatakia heri ya Kristimas na mwaka mpya, pamoja na kutuma kitu chochote ili wafurahie,sababu familia ni sehemu ya kwanza ambayo inatengeneza msingi wa amani yako.
Vibe baada ya Uzinduzi wa kampeni ya selebretika Kijamukaya 
Vinywaji vyenye chapa ya selebretika Kijamukaya 

Post a Comment

0 Comments