JAJI Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania,Dkt. Mustapher Mohamed Siyani ameipongeza Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), kuendeIea kutoa elimu kuhusu madhara yatokanayo na dawa za kulevya na namna ambavyo watanzania wanaweza kujiepusha kujiingiza katika matumizi ya dawa hizo.
Ametoa pongezi hizo Januari 29, 2025 alipotembelea banda la Mamlaka hiyo katika Maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea kufanyika kitaifa viwanja vya Nyerere ‘Square’ jijini Dodoma amesema dawa za kulevya si kitu ambacho mtu yoyote anapaswa kukipunzia pengine ni ngumu kuelewa hata dawa za hospitali zinazozaniwa kwamba ni dawa salama na zenyewe zinaweza kusababisha uraibu ndani yake.
Pia amewataka wananchi wa Mkoa wa Dodoma na mikoa ya jirani kutembelea banda la Mamlaka hiyo ili waweze kupata elimu kuhusu madhara yatokanayo na matumizi ya dawa za kulevya.
Ameeleza kuwa watu wengi hawajui kama zinaweza kujenga uraibu na baadaye na kusababisha matatizo.
Jaji Kiongozi huyo amesema ni jambo muhimu kwa mamlaka kuendeleza kuwa karibu na mahakama hususani katika kuhudhuria mafunzo.
"Niwapongeze kwa kujitangaza kufanya watanzania wajue madhara ya dawa za kulevya,mimi nimepata fursa ya kupata elimu, nilikuwa nasikia Skanka, kumbe Skanka ni hatari kuliko kile cha Arusha," amesema.
Ameongeza kuwa kwa pande zote mbili mahakama na mamlaka hiyo ni vema kuendeIea kujifunza mambo yanayotokea mahakamani wakati wa uendeshaji wa mashauri yanayohusu dawa za kulevya pamoja na kujifunza sheria mbalimbali zinazohusu dawa hizo Kila wakati.
Aidha amefurahishwa kupata elimu na kwamba kile ambacho kimesemwa, taarifa zinazotolewa na DCEA wanaonesha wanafanya kazi huku akiendelea kutoa pongezi zake kwa mamlaka hiyo.
Jaji Kiongozi amesema kuwa maonesho hayo ni muhimu kwa lengo la kutoa elimu huku akiwataka wananchi wa Mkoa wa Dodoma na mikoa ya jirani kutembelea banda la Mamlaka hiyo ili waweze kupata elimu kusudiwa.
Amesema kila mwananchi anajukumu la kuhakikisha nchi inakuwa salama na kwamba kila mtanzania anakuwa na uwezo wa kufanya kazi na kuzalisha kipato kwa kuleta maendeleo.
"Tukitazama Dira ya Tanzania miaka 25 ijayo lazima nchi yetu iwe salama na haziwezi kuwa salama kama watanzania wengi wamejiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya.
Awali Afisa elimu kwa jamii, Anna Tengia amesema kuwa lengo la kuwepo kwenye maonesho hayo ni kutoa elimu na namna ya watu kujiepusha katika dawa hizo.
" Tupo hapa kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu madhara yatokanayo na dawa za kulevya, na ni namna gani watu wanajiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya na namna ya kujiepusha katika dawa hizi," amesema.
Ameongeza kuwa katika banda hilo wapo na sampuli mbalimbali za dawa za kulevya pamoja na muungozo wa kutoa elimu.
Mhe Jaji Kionongozi ameeleza kuwa uwepo na dawa tiba zenye asili ya kulevya zilizoruhusiwa kwa matibabu ya binadamu ambazo zikitumika bila maelekezo ya daktari zinakwenda kusababisha uraibu kama ule wa watumiaji wa dawa nyingine za kulevya.
0 Comments