Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Kenan Kihongosi,akifungua Kliniki ya Samia Teacher's Mobile Clinic inayoratibiwa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kwa kushirikiana na Serikali.
Na Mwandishi wetu Amo Blog Simiyu
Walimu zaidi ya 2,500 Mkoa wa Simiyu wamejitokeza kwa wingi kuhudhuria Kliniki ya Samia Teacher's Mobile Clinic inayoratibiwa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kwa kushirikiana na Serikali.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kliniki hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Kenan Kihongosi, amewataka walimu Mkoani humo kushirikiana na kudumisha umoja,ili kuepuka migawanyiko inayoweza kuathiri ustawi na utendakazi wao.
Mhe.Kihongosi amesema kuwa Kliniki ya Samia ni sehemu muhimu ya kutatua changamoto zinazowakabili walimu na inatokana na maono ya Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha kuwa walimu wanafanya kazi katika mazingira bora hali itakayo saidia kuinua kiwango cha elimu nchini.
Aidha Mhe.Kihongosi amewataka maafisa utumishi kubadilika katika utoaji wa huduma kwa walimu na kueleza kuwa hatomvumilia afsa yeyote anaye shindwa kutatua changamoto za mwalimu kwa visingizio mbalimbali huku akiagiza hatua kali za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya maafisa wanaoshindwa kufuata sheria, kanuni na taratibu wakati wa utoaji wa huduma kwa umma.
Hatahivyo Mhe.Kihongosi akitoa ufafanuzi kuhusu changamoto zinazo wakabili walimu amewaomba walimu kuendelea kuiamani Serikali na kuipa muda wa kutatua changamoto zao, kuliko kufanya kazi kwa kinyingo na kupunguza morali ya utendakazi wao
Naye Makamu wa Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Seleiman Ikomba, akitoa salamu za CWT ameelezea uwepo wa Tabia ya baadhi ya maafisa utumishi wanao waonea walimu nakushindwa kutatua changamoto zao kwa visingizio mbalimbali huku akiipongeza Serikali ya Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwa usikivu na kujali maslahi ya wafanyakazi, hali iliyo sababisha Kliniki hiyo kupewa jina la Samia Teachers Mobile Clinic ikiwa ni sehemu ya kuonyesha uungaji mkono wa Serikali.
Ikomba amefafanua kuwa Mkoa wa Simiyu umekuwa mkoa wa 17 kushiriki Kliniki ya Samia, na kwamba katika mikoa mingine, Kliniki hiyo imekuwa na mafanikio makubwa kama ilivyo kuwa katika mkoa huo.
Kwa upande wake Mwalimu Said Abdallah, mmoja wa walimu walioshiriki Kliniki hiyo, amesema kuwa Kliniki ya Samia imekuwa ni suluhu kwa changamoto nyingi zinazowakabili walimu, kwa kuwa walimu wanaajiriwa kila mwaka, ni muhimu Kliniki hiyo ikawa endelevu ili kutoa majibu ya changamoto za walimu.
Baadhi ya Viongozi wa CWT Taifa waliofika mkoani Simiyu Kwa ajili ya utatuzi wa changamoto za walimu. 
Walimu waliojitokeza katika Mkoa wa Simiyu kwa ajili ya huduma ya Samia Teacher's Mobile Clinic inayoratibiwa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kwa kushirikiana na Serikali.
Walimu waliojitokeza katika Mkoa wa Simiyu kwa ajili ya huduma ya Samia Teacher's Mobile Clinic inayoratibiwa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kwa kushirikiana na Serikali wakiendelea kupatiwa huduma.

1 Comments
Kliniki hiyo ifanyie pia changamoto za madai ya Wastaafu
ReplyDelete