
Mgombea Udiwani Mteule Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Mjini ,Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Salum Kitumbo, amechukua Fomu za Uteuzi za kugombea nafasi ya Udiwani zilizotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) katika ofisi za kata ya mjini .
Fomu hizo zimetolewa leo Jumanne Agosti 19,2025 na Msimamizi wa Uchaguzi kata ya Mjini Mashishanga.
Tukio hilo limeashiria kuanza kwa mchakato wa kuomba ridhaa ya kuwatumikia wananchi katika kata ya mjini.
Baada ya kuchukua fomu hiyo, Mhe.Kitumbo ameahidi kuendelea kuwatumikia wananchi wa kata hiyo kwa moyo wa dhati na bila kuchoka, huku akisisitiza lengo lake la kuchochea maendeleo kupitia shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi.
Aidha, amesisitiza kuwa yote atakayofanya yataendana na Ilani na maelekezo ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), akiahidi kushirikiana kwa karibu na chama chake na wananchi kuhakikisha kila hatua inachangia maendeleo ya kata.
Pia,amewaomba wananchi kuendelea kumpa ushirikiano wakati atakaporejesha fomu yake na katika kipindi chote cha uchaguzi mkuu, akiahidi kushirikiana nao kwa karibu ili kuhakikisha maendeleo ya kata ya mjini yanaendelea na kila mwananchi anaona matokeo chanya ya maendeleo.




0 Comments