6/recent/ticker-posts

RC MHITA AWASISITIZA WANANCHI KUJIUNGA NA MFUKO WA BIMA YA AFYA KWA WOTE,MKURUGENZI MIPANGO NHIF NA MENEJA TIRA TABORA WATOA ELIMU KWA WADAU

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Mboni Mhita akifungua Mafunzo ya Bima ya Afya kwa wote kwa Watumishi na Wadau wa Sekta ya Afya Wilaya ya Shinyanga na Kishapu.

Na Mwandishi Wetu Amo Blog Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mboni Mhita amewahimiza wananchi mkoani hapa kujiunga kwenye mfuko wa Bima ya Afya kwa wote utakaowawezesha watu wa makundi yote kunufaika na huduma za uhakika, bora, gharama nafuu na haraka zaidi.

Ameyasema hayo leo Disemba 17, 2025 wakati akifungua Mafunzo ya Bima ya Afya kwa wote kwa Watumishi na Wadau wa Sekta ya Afya Wilaya ya Shinyanga na Kishapu, mafunzo yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Akifungua mafunzo hayo, Mhe. Mhita amesema Serikali itakuwa mstari wa mbele kuhamasisha wananchi, Watumishi wa Taasisi za Umma na Binafsi kujiunga kwenye mfuko wa Bima ya Afya ili kuhakikisha zinaenda kuwa suluhisho kwa kupunguza malalamiko, kupunguza sintofahamu ya gharama na kuondosha mzigo wa lawama kwa watoa huduma.

“Mfuko wa Bima ya Afya ni suluhisho sahihi la kupunguza malalamiko, sintofahamu na lawama baina ya wananchi na watoa huduma. Ninawasihi Wnanchi na Watumishi wa Taasisi za Umma na Binafsi kujiunga kwenye mifuko hii ambayo itawarahisishia kupata huduma bora kwa uharaka zaidi” alisema RC Mhita.

Aidha Mhe. Mhita amewataka wadau wa Sekta ya Afya kushirikiana kwa pamoja kutoa elimu kwa wananchi na makundi mbalimbali kuhusu umuhimu wa kujiunga na mifuko ya Bima za Afya ili kutekeleza maagizo ya Mhe. Rais ya kuhakikisha ndani ya siku 100 huduma ya Bima inapatikana kwa watu wote.

Kwa upande wake Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudasi Ndungile, amesema huduma ya Bima ya Afya kwa wote inaenda sambamba na matumizi ya Tehama ikiwemo kujisajili kwenye mfumo wa TIRA na GOT HOMIS ambayo itasaidia kupunguza rushwa, kupokea fedha nje ya mfuko na kupunguza malalamiko ya wananchi.

Naye Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bw. Selestine Muganga amesema kuwa Serikali inatambua hali mbalimbali za kiuchumi za wananchi, hivyo kwa familia zenye hali duni ya kiuchumi, Serikali itawalipia gharama za Bima ya Afya kwani tayari imefanya utambuzi kupitia mamlaka za utambuzi (TASAF).

Kwa upande wake, Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Kanda ya Magharibi Bi. Awanje Matenta, amesema mpaka sasa Vituo vya Afya 171 vimesajiliwa sawa na asilimia 80% ambavyo vitasaidia katika utoaji wa huduma za Bima ya Afya, ikiwa ni hatua ya awali ya utekelezaji wa Sheria ya Huduma bora ya Afya kwa wananchi.
Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudasi Ndungile, akitoa elimu ya huduma ya Bima ya Afya kwa wote kwa washiriki wa mafunzo ya mfumo huo.
Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bw. Selestine Muganga akitoa elimu kwa washiriki wa mafunzo hayo.
Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Kanda ya Magharibi Bi. Awanje Matenda,akitoa salamu za TIRA kwa washiriki wa mafunzo hayo.
Watumishi na Wadau wa Sekta ya Afya Wilaya ya Shinyanga na Kishapu wakipata mafunzo.
Watumishi na Wadau wa Sekta ya Afya Wilaya ya Shinyanga na Kishapu wakipata mafunzo.
Watumishi na Wadau wa Sekta ya Afya Wilaya ya Shinyanga na Kishapu wakipata mafunzo.
Watumishi na Wadau wa Sekta ya Afya Wilaya ya Shinyanga na Kishapu wakipata mafunzo.
Watumishi na Wadau wa Sekta ya Afya Wilaya ya Shinyanga na Kishapu wakipata mafunzo.
Mwita Thimas mmratibu wa elimu ya afya kwa umma mkoa wa Shinyanga akizungumza na wa shiriki.

Post a Comment

0 Comments