Mhe.Diwani wa Kata ya Ngokolo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Jackline Isaro amewahidi Wananchi wa Kata hiyo, kuendelea kuleta maendeleo zaidi ikiwa ni pamoja kusikiliza kero za Wananchi katika mitaa yote inayounda kata hiyo.Jackline amebainisha hayo kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika Mtaa wa Ngokolo ukiwa ni muendelezo wa mikutano yake anayo endelea kuifanya mtaa kwa mtaa kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitaftia ufumbuzi kupita wataalam anao ambatana nao kutoka kwenye kata.
Amesema, Kiongozi anayewafikia watu na kujua changamoto zao ndiye anaweza kuleta maendeleo kwa haraka kuliko yule anayependa kukaa Ofisini, hivyo Kata ya Ngokolo itegemee kuona maendeleo kwa kasi.
Aidha ameeleza kuwa kupitia mfuko wa jimbo Mhe,Mbunge Patrobas Katambi ametoa fedha kwa ajili ya kuanzisha ujenzi wa zahanati katika kata hiyo sambamba na kuelezea mkakati wa serikali katika kuhakikisha wanatengeneza barabara zilizo haribika katika mitaa hiyo.
“sitakuwa kiongozi wa kukaa ndani, nitashirikiana na viongozi wa serikali za mtaa kufanya mikutano ya hadhara kila baada ya miezi mitatu kusikiliza kero zenu na kuzipatia ufumbuzi na hatimaye kuwaletea maendeleo,“ amesema Jackline.
Ameongeza kuwa anazifahamu changamoto zinazowakabili Wafanyabishara wa soko la mitumbani lililopo katika kata hiyo na kwamba atazifanyia kazi, ili waweze kufanya kazi kwautulivu na kuendelea kuimarisha uchumi wao.
Akizungumzia mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri, Jackline amesema kuwa ataendelea kupambana ili kuhakikisha walengwa wanaipata mikopo na kujikwamua kiuchumi.

0 Comments