6/recent/ticker-posts

MBIO ZA BAISKELI ZAPAMBA MOTO BUSIYA MAANDALIZI YA TAMASHA LA SANJO YA BUSIYA 2026

BUSIYA YAANZA NA MBIO ZA BAISKELI KUELEKEA TAMASHA LA SANJO YA BUSIYA 2026


Zikiwa zimesalia siku 2 kufanyika kwa kilele cha Tamasha la Sanjo ya Busiya litakalofanyika julai 7 katika viwanja vya ikule ya Busiya ukenyenge Kishapu mkoani Shinyanga ,uongozi wa utemi huo umefanya kwa mara ya kwanza Mbio za Baiskeli kwa Lengo la kurejesha utamaduni wa Baiskeli kwa kabila la wasukuma.




Mbio hizo zimefanyika jumamosi ya Julai 04 ambapo mashindano yalianzia Kolandoto hadi ikulu ya Busiya na washiriki walipokelewa na Mtemi wa Busiya Ntemi Makwaia wa iii pamoja na machifu wengine kutoka meeneo mbalimbali.


Kufanyika kwa mbio hizo ni ishara ya shamrashamra za Tamasha la Sanjo ya Busiya ambalo litazinduliwa rasmi Julai 05 na hitimisho ni Julai 07 ambapo ngoma mbalimbali kutoka Busiya na nchi jirani zitashiriki.

Post a Comment

0 Comments