
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga (KASHWASA) leo, Oktoba 15, 2026, imekutana na wateja wake kujadili mapendekezo ya mabadiliko ya bei za maji kwa kipindi cha miaka mitano, kuanzia mwaka wa fedha 2026/2027 hadi 2030/2031.
Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa KASHWASA uliopo mjini Shinyanga na kuwakutanisha wateja wa mamlaka hiyo kutoka mikoa ya Geita, Simiyu, Mwanza, Shinyanga, Tabora na Singida, wakiwemo mamlaka za maji, vyombo vya watoa huduma ya maji ngazi ya jamii na migodi.
Akifungua kikao hicho, Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga, ameipongeza KASHWASA kwa kuendelea kutoa huduma ya uhakika kwa wateja wake licha ya changamoto zinazoikabili mamlaka hiyo, ikiwemo madeni makubwa inayodai wateja wake.
Akifafanua lengo la mapendekezo ya kuongeza bei za maji, Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA, Mhandisi Justine Rujomba, amesema hatua hiyo inalenga kuboresha uzalishaji na usambazaji wa maji safi na salama kwa wateja wake.
Katika kikao hicho, bei za maji kwa mwaka wa fedha 2026/2027 zilipitishwa kuwa shilingi 1,401 kwa kila mita ya ujazo kwa mamlaka za maji (WSSAs), kutoka shilingi 985; shilingi 1,053 kwa vyombo vya watoa huduma ya maji ngazi ya jamii (CBWSOs), kutoka shilingi 740; na shilingi 1,764 kwa migodi, kutoka shilingi 1,240.
Kaimu Mkurugenzi wa KASHWASA, John Nzengo akizungumza kwenye kikao hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA, Mhandisi Justine Rujomba akizungumza kwenye kikao hicho.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga akizungumza kwenye kikao hicho.
Picha ya pamoja.









0 Comments