6/recent/ticker-posts

KOM SCHOOLS YAIBUKA MSHINDI KIPENGELE CHA BEST PRIVATE SCHOOL ,TUZO ZA MDAU SHUPAVU AWARDS – SHINYANGA 2026




Washindi wa MDAU SHUPAVU Awards – Shinyanga 2026, Season 2, wametangazwa baada ya mchakato wa upigaji kura za wazi, huku jumla ya washindi 60 wakitajwa katika kategoria mbalimbali zinazogusa biashara, ujasiriamali, habari, burudani, huduma, ubunifu na mchango kwa jamii.

Tuzo hizo zimewakutanisha wadau kutoka sekta mbalimbali ndani ya Mkoa wa Shinyanga, huku washindi wakipatikana kupitia kura za wananchi na wadau, katika mchakato uliolenga kutambua kazi, ubunifu, ushawishi na mchango unaotolewa katika jamii.

Miongoni mwa washindi waliotangazwa katika 
Sekta ya elimu KOM Schools imeibuka mshindi katika kipengele cha Best Private School, huku Kahama College ikiibuka katika kipengele cha – Best Science College, na Kolandoto College –ikiibuka mshindi katika kipengele cha  Outstanding Science Education College.

Katika sekta ya habari na mawasiliano, Ibrahim Haruna ametangazwa mshindi wa Best Male Media Personality, huku Neema Nkumbi akishinda tuzo ya Best Female Media Personality.

Kwa upande wa burudani, Level One Pub imetajwa kuwa mshindi wa Best Community & Recreation Spot, MC Dizzoo akishinda Best Male MC, huku DJ Mshedede akitwaa tuzo ya Best DJ. Kambi ya Nyani imeibuka mshindi katika kategoria ya Best Entertainment Group.

Washindi wengine ni Junior Montana – Best Public & Community Photographer, Kichomi Music Sound – Best Music, Sound & Entertainment Service Provider, Savco Fashion – Best Content Creator, na Nyasani – Best Artist Influencer.

Katika biashara na huduma, Shigaka Luxury Bus – Kahama imeshinda Best Transport & Logistics Service Provider, High Classy Events – Best Bridal & Event Styling Service, Kichomi Events Planners – Kahama – Best Decoration Service Provider, huku JJ Cosmetics ikishinda Best Cosmetics Service Provider.

Aidha, Adam Furniture imeshinda Best Furniture Service Provider, Jambo Bakery – Best Bakery & Snacks Service Provider, Naipa Films – Best Cinematographer, huku MC Rose – Kahama akishinda Best Female MC.

Katika sekta ya mitindo na urembo, washindi ni pamoja na Halima Designer – Kahama – Best Female Fashion Designer & Tailor, Mika Designer – Best Male Fashion Designer & Tailor, Gvenwear – Shinyanga – Best Creative Fashion Brand & Designer, Lee Beauty & Braids – Best Salonist & Creative Hairstylist, na Vai Hair Beauty Saloon – Best Makeup Artist.

Kwa upande wa ushawishi na mchango kwa jamii, Norah_Jewellry ameshinda Best Female Social Impact Influencer, Mr Laza (Msanuaji) – Most Influential Public Figure, Rose John Mwitumba – Best Entrepreneur & Business Leader, na GAET-Tanzania – Best Youth Empowerment Initiative.

Washindi wengine katika orodha hiyo ni Joseph Jisena – Budagala Gold Plant aliyeshinda Outstanding Gold & Mining Services, Wahit ime Company Ltd – Best Social Impact Company, Joxedaver Company Ltd – Outstanding Community Impact Company, Muna & Coesta INV Limited – Best Innovative Business/Company, pamoja na Jamukaya (Jambo Group) – Best Brand of the Year.

Katika kategoria za vyombo vya habari, Jambo FM imetajwa kuwa mshindi wa Best FM Radio Station, huku Gold FM Digital ikishinda Best Digital Media Platform.

Pia, Mhe. Hamza Yusuf Tandiko ameshinda Outstanding Leadership in Mining & Community Development, huku William Bundala (MC Kijukuu) akitunukiwa Special Recognition for Community & Social Impact. MC Mama Sabuni ameibuka mshindi wa Best Female Social Impact Influencer.

Tuzo hizo ni sehemu ya kutambua na kuenzi juhudi za watu, taasisi na biashara zinazotoa mchango katika maendeleo ya jamii na kukuza shughuli mbalimbali ndani ya Shinyanga.

MDAU SHUPAVU Awards – Shinyanga 2026, Season 2, imefanyika chini ya kaulimbiu ya kutambua wadau kupitia kura za wazi, huku washindi wakipatikana katika jumla ya kategoria 60.

Kwa washindi wote, tuzo hizi ni utambuzi wa kazi na mchango wao; kwa washiriki wengine, mchakato huo umeendelea kuonyesha nafasi ya ubunifu, ujasiriamali na huduma mbalimbali katika kukuza jamii ya Shinyanga.

MDAU SHUPAVU AWARDS – SHINYANGA 2026 | SEASON 2
Winners kupitia kura za wazi
HOLYSMILE

Post a Comment

0 Comments