6/recent/ticker-posts

NHIF SHINYANGA TUNASEMA USISUBIRI KUUGUA ,JIUNGE NA FAHARI AFYA – BIMA YA AFYA KWA WOTE!


Je, unajua kuwa kwa shilingi 150,000 tu kwa mwaka, unaweza kuandikisha familia yako ya watu 6 na kupata huduma mbalimbali za matibabu?

Kupitia Bima ya Afya ya Fahari Afya, wewe na familia yako mnapata fursa ya kunufaika na huduma zifuatazo:

✅ Kuonana na daktari.
✅ Huduma za dawa na vitendanishi.
✅ Vipimo vya maabara.
✅ Huduma za radiolojia.
✅ Huduma za upasuaji.

Unapata huduma za matibabu kuanzia ngazi ya zahanati, kituo cha afya, hospitali za wilaya, hospitali za rufaa hadi hospitali za taifa, kulingana na utaratibu na masharti ya kifurushi.

TAFAKARI KIDOGO!

Bila kuwa na bima ya afya, unaweza kutumia hadi shilingi 200,000 kwa siku moja unapohitaji matibabu.

Kwa nini usijiunge na Fahari Afya kwa shilingi 150,000 tu kwa mwaka na kuandikisha familia yako ya watu 6?

Usisubiri kuugua ndipo utafute fedha za matibabu. Chukua hatua leo!

FAHARI AFYA – BIMA YA AFYA KWA WOTE!

JIUNGE, WAKATI NI SASA!

AFYA YAKO, MTAJI WAKO!

Post a Comment

0 Comments