6/recent/ticker-posts

DC SAMIZI ASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA, AWAPA MAJUKUMU MAZITO WAZAZI NA WALEZI.





Na Marco Maduhu, SHINYANGA

HALMASHAURI ya Manispaa ya Shinyanga mkoani humo  imeadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika, huku Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akiwataka wazazi  na walezi kutumia Teknolojia kwa maendeleo endelevu na siyo kusababisha Mmomonyoko wa Maadili.

Maadhimisho  ya siku ya Mtoto wa Afrika Manispaa ya Shinyanga yamefanyika leo Juni 15, 2023 katika Viwanja vya Sabasaba, ambapo kilele chake Kitaifa na Mkoa wa Shinyanga kitafanyika kesho Juni 16.

Samizi akizungumza kwenye Maadhimisho hayo, amewataka wazazi na walezi kutumia Teknolojia kwa maendeleo endelevu na siyo kusahau malezi bora ya watoto kuliko  kuwa bize na mitandao, na hatimaye kusababisha Mmomonyoko wa Maadili.

“Ulimwengu huu wa digital unafursa mbalimbali endapo ukitumika vizuri kwa maendeleo endelevu, lakini ukitumika vibaya ndiyo chanzo kikuu cha Mmomonyoko wa maadili kwa watoto,”amesema Johari.

Aidha, amewataka pia wazazi wasiruhusu watoto wao wakuchezea simu za wakubwa, huku akiwasihi pia wawe makini na maudhui ya ‘Cartoon’ ambazo wana angalia watoto ili kutoiga mambo ya ajabu ambayo ni kinyume na maadili ya Mwafrika.

Katika hatua nyingine Johari Samizi amewataka watoto kutokubali kushikwa shikwa katika maungo yao, na mtu ambaye akiwafanyia vitendo hivyo watoe taarifa kwa Walimu, Wazazi, Maofisa Maendeleo, Ustawi au kwa kiongozi yoyote wa Serikali ili achukuliwe hatua.

Naye mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, amesema Serikali itaendelea kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vya ukatili, pamoja na kuunda Mabaraza ya watoto ambayo husaidia kupasa sauti za vitendo vya ukatili.

Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Manispaa ya Shinyanga Grace Ngowi akisoma taarifa ya watoto kwenye Maadhimisho hayo, amewaomba viongozi wa Serikali kuendelea kuwajibika ipasavyo juu ya kuzuia vitendo vya ukatili dhidi ya watoto wadogo, pamoja na kuharakisha utolewaji wa hukumu kwa watu ambao wameshitakiwa kufanya vitendo hivyo.

Kauli Mbiu ya mwaka huu ya Maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika inasema ‘zingatia usalama wa watoto katika ulimwengu wa kidigital.’


Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko.




Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi.



Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi (kulia)akipokea picha yake ambayo imechora wa vijana wa Commpasion kutoka Kanisa la AICT Kitangili.








Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi (katikati) akiwa na Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko (kulia) pamoja na Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii John Tesha, wakipokea Maandamano.





Post a Comment

0 Comments