6/recent/ticker-posts

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA, DKT. DAMAS NDUMBARO ABISHA HODI SHINYANGA ,ATANGAZA VITA KWA WATUMISHI WANAO PINDISHA HAKI.






Waziri wa katiba na Sheria Dr.Damasi Ndumbaro akitatua mgogoro wa familia ulio dumu kwa miaka nane Kishapu.







Waziri wa katiba na Sheria Dr.Damasi Ndumbaro akiwa ofisini kwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga na mwenyeji wake Mhe.Christina Mndeme .





Mhe.mkuu wa mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akitoa taarifa ya utekelezaji wa kampeni ya Mama Samia legal Aid Campaign kwa wa Waziri wa Katiba na Sheria nchini Dkt. Damas Ndumbaro




NA AMO BLOG






Waziri wa Katiba na Sheria nchini Dkt. Damas Ndumbaro amefanya ziara ya kikazi mkoani Shinyanga kwa lengo la kukagua utekelezaji wa kampeni ya huduma ya msaada wa kisheria ya Mama Samia legal Aid Campaign.

Waziri Ndumbaro amefanya ziara hiyo leo Juni 15, 2023 mkoani
Shinyanga kisha kukutana na watumishi katika ofisi ya mkuu wamkoa ambapo pamoja na mambo mengine ameahidi kuanza kuwachukulia hatua baadhi ya watendaji walio pewa dhamana ya kusimamia sheria na kupindisha sheria kwa kutozingatia misingi na taratibu ya kazi yao hali inayo changia uwepo wa ongezeko la migogoro ya ardhi katika maeneo mbalimbali nchini.



Aidha Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro umeupongeza uongozi wa Mkoa wa Shinyanga kwa kufanya vizuri kwenye kampeni ya Mama Samia legal Aid Campaign huku akieleza kuwa kampeni hiyo itapita kwenye mikoa yote ya nchini na kuwafikia wananchi kwenye wilaya zao ikiwa ni pamoja na kupita katika kata na vijiji hali itakayo saidia kumaliza changamoto zinazo wakabili wananchi wanyoge kwa kutofahamu sharia na wengine kukosa haki kutokana na kukosa uwezo wakuweka wanasheria wakuwasaidia kuendesha kesi zao.

“Kampeni hii ambayo imepewa heshima kubwa kwa kupewa jina la kiongozi wetu mkuu wa nchi inatokana na ilani ya Chama Cha Mapinduzi ambayo imeagiza waananchi wapate elimu ya sheria na msaada wa sheria ,kampeni hii ni maelekezo ya Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hasani ndipo wizara ikaamua kuja na kampeni hii na hivyo niwapongeze Mkoa wa Shinyanga kwa kuendelea kutoa vizuri huduma ya msaada wa kisheria ”,



Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa kampeni ya Mama Samia legal Aid Campaign ngazi ya mkoa mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme amesema kampeni hiyo imekuwa msaada mkubwa katika kutatua migogoro iliyokuwa ikitokana na ukosefu wa elimu ya masuala ya sheria huku akieleza miongoni mwa sababu zinazopelekea ongezeko la migogoro ni uwepo wa tabia ya baadhi ya watumishi kukosa maadili ya misingi na taratibu ya kazi yao ikiwemo kupindisha sharia na kuwafanyawananchi wakukosa haki.

“Mara baada ya kuanzishwa kwa kampeni hii ya msaada wa kisheria imekuwa ni mkombozi mkubwa kwenye jamii kwa kupunguza migogoro ya ardhi, urithi na mambo mengine yanayohusiana na sheria Kupitia kampeni hii dhuruma waliokuwa wakikumbana nayo wananchi na kukosa haki zao sasa inakwenda kuisha kwani mpaka sasa malalamiko yamepungua, Tunamshukuru sana Mhe. Rais kwa kutuletea kampeni hii ndani ya mkoa tunaahidi kuendelea kutoa ushirikiano ili malengo ambayo serikali imejiwekea yaweze kufikiwa”, amesema RC Mndeme.

Pia RC Mndeme amemuomba waziri wa katatiba na Sheria kupitia upya vifungu vya sheria vinavyotoa dhamana kwa wanaokutwa na hatia ya kujihusisha na vitendo vya ubakaji na ulawiti kwani imekuwa chanzo cha kujirudia kwa matukio ya vitendo hivyo.



Waziri wa katiba na Sheria Dr.Damasi Ndumbaro akipokelewa mkoani Shinyanga Baada ya kuwasiri.









Mkuu wawilaya ya Kahama Mhe.Mboni Mhita akisikiliza kwa umakini maelekezo ya Waziri wa katiba na Sheria Dr.Damasi Ndumbaro akiwa katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga.








Waziri wa katiba na Sheria Dr.Damasi Ndumbaro akitoa maelekezo juu ya kampeni ya huduma ya Msaada wa Kisheria.



Wataalamu kutoka wizara ya katiba na sheria wakisikiliza maelekezo ya waziri mwenye dhamana.




Waziri wa katiba na Sheria Dr.Damasi Ndumbaro akitatua mgogoro wa familia ulio dumu kwa miaka nane katika kijiji cha Wishiteleja kilichopo katika kata ya Mondo Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.





Waziri wa katiba na Sheria Dr.Damasi Ndumbaro akitatua mgogoro wa familia ulio dumu kwa miaka nane katika kijiji cha Wishiteleja kilichopo katika kata ya Mondo Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga. in





Waziri wa katiba na Sheria Dr.Damasi Ndumbaro akisikiliza mgogoro wa familia ulio dumu kwa miaka nane katika kijiji cha Wishiteleja kilichopo katika kata ya Mondo Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.




Wataalamu kutoka wizara ya katiba na sheria wakisikiliza maelekezo ya waziri mwenye dhamana akizungumza na wananachi wa katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya maganzo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.












Waziri wakatiba na Sheria Dr.Damasi Ndumbaro akisikiliza kero za wananchi wa kata ya Magazo walio jitokeza na kuuliza maswali mbalimbali wakihitaji kupata ufumbuzi.




wananchi wa kata ya Magazo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga wakimsikiliza waziri wakatiba na sheria kwenye mkutano wa hadhara.





wananchi wa kata ya Magazo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga wakimsikiliza waziri wakatiba na sheria kwenye mkutano wa hadhara.





wananchi wa kata ya Magazo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga wakimsikiliza waziri wakatiba na sheria kwenye mkutano wa hadhara.

Post a Comment

0 Comments