6/recent/ticker-posts

MBUNGE JIMBO LA MSALALA MHE.IDD KASSIM IDD ATOA OMBI WIZARA YA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO .

 Mbunge wa jimbo la Msalala Mhe.Idd Kassim akichangia bajeti ya

wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo 

bungeni .

 CHANZO MICHUZI  BLOG .

 

Mbunge wa jimbo la msalala Mhe.Idd Kassim Idd ameiomba wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kutembelea mikoani na kuona vipaji vilivyopo ili waweze kuviibua na kuviendeleza . 

Mhe.amesema kuwa mikoani kunavipaji vingi hivyo nivema maafsa utamadini wakatambua vipaji hivyo na kuviendeleza hali itakayo saidia kuchochea maendeleo kwa wanamichezo wenyewe ,serikali na Taifa kwa ujumla.

Aidha Bunge limepitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Shilingi 35,445,041,000 ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kwa lengo la katika kuwahudumia Watanzania.

 

Wabunge wamefikia uamuzi huo Bungeni, Juni 6, 2023 mchana jijini Dodoma mara baada ya kujadili mpango wa Wizara hiyo uliowasilishwa na Waziri Balozi Dkt. Pindi Chana.

 

Pia Balozi Dkt. Chana amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia Tanzania kushirikiana na Kenya na Uganda kuomba kuwa mwenyeji wa Mashindano ya Mpira wa Miguu barani Afrika (AFCON 2027) ambayo ni mashindano mkubwa barani Afrika.

 

Kwa upande wake Naibu Waziri Mhe. Hamis Mwinjuma akifafanua hoja ya Mbunge wa Makete Festo Sanga kuhusu ujenzi wa viwanja vya michezo, amesema kuwa kampuni zinazotekeleza miradi mikubwa nchini zinatakiwa kutumia sehemu ya mapato yao kurudisha kwa jamii (CSR) ili kusaidia kutengeneza miundombinu ya michezo nchini kutoka katika sekta za fedha, nishati na madini na tayari Wizara imeanza kufanya mawasiliano na Wizara husika na mawasiliano yanaendelea vizuri hatua inayosaidia kufikia malengo ya Serikali.

 

Akichangia mjadala kwenye bajeti hiyo, Mbunge wa Bunda Mjini Mhe. Ester Bulaya amesema kuwa Wizara hiyo ina bajeti ndogo hivyo waongezewe hela, itatengeneza ajira mpya, ikipewa fedha za kutosha taifa litakuwa na furaha kwa kuwa Watanzania wanapenda michezo ili kupata viwanja bora na timu imara ambazo zitakuwa na ushindani katika uga wa kimataifa.


Waziri wa wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.Waziri Balozi Dkt. Pindi Chana 

Post a Comment

0 Comments