6/recent/ticker-posts

RC MNDEME AZINDUA RASMI KAMPENI YA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN SHINYANGA ,WADAU WAMPONGEZA RAIS SAMIA.







Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (wa pili kulia) akizindua Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign”

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign.


NA MALUNDE BLOG


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amezindua Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” inayotokana na azma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha kwamba msaada wa kisheria unatolewa kwa wananchi wote ili kupata haki, usawa, amani na maendeleo.




Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo leo Jumapili Juni 11,2023 katika uwanja wa Sabasaba Mjini Shinyanga, Mndeme ameiahidi Wizara ya Katiba na Sheria na wadau inaoshirikiana nao katika kuendesha kampeni ya kitaifa ya msaada wa kisheria - Mama Samia Legal Aid Campaign kutoa ushirikiano wa hali na mali katika kufikia malengo ya kampeni hiyo ya kutoa msaada wa kisheria kwa watanzania wote hasa wale waishio maeneo ya pembezoni.




Amesema lengo kuu la kampeni hiyo ni kulinda na kukuza upatikanaji wa haki kwa wote kupitia huduma ya msaada wa kisheria nchini hivyo akaagiza kata zote zihakikishe zinatenga maeneo maalum ambayo watoa huduma wataweza kuongea na mwananchi mmoja mmoja kwa faragha.




“Kampeni hii ni utekelezaji wa Katiba yetu. Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 imetambua umuhimu wa upatikanaji haki kwa wananchi kwa kuwa Ibara ya 231(k) ya Ilani imetuelekeza “kuimarisha huduma za msaada wa kisheria hususan kwa wanawake na Watoto katika maeneo yote”, amesema Mhe. Mndeme.




Amesema Kampeni hiyo imekuja katika muda muafaka kwani wananchi wa Shinyanga wana uhitaji mkubwa wa msaada wa kisheria katika nyanja tofauti hususan kuelewa haki zao, wajibu wao, namna ya kutatua migogoro ya ardhi, ndoa, masuala ya mirathi, wosia na utawala bora.





Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.







Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Dkt. Christina Mzava akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.






Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
















































































Post a Comment

0 Comments