6/recent/ticker-posts

JAMBO FM YA ZINDULIWA RC MNDEME ASHIRIKI ZOEZI LA UPANDAJI MITI SHINYANGA.

l



Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akimwagilia mti alio upanda.


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza na Meneja wa Radio kutoka jambo fm.



Meneja wa Jambo fm akitoa neno la Shukrani mbelea ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme.





NAMWANDISHI WETU AMO BLOG SHINYANGA.



Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amefanya uzinduzi wa kituo cha matangazo Jambo fm na kushiriki zoezi la upandaji miti katika eneo la bustani ya kupumzikia NBC ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya sikukuu ya JAMUKAYA .

Mhe.Mndeme akishiriki zoezi hilo ameipongeza Jambo FM inayorusha matangazo yake kutoka katika Manispaa ya Shinyanga kwa kazi kubwa na nzuri ya kuhabarisha na kuelimisha jamii juu ya mambo mbalimbali yanayo fanywa na mkoa huo.


Awali akimkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi amesema kuwa, Jambo FM wamekuwa wadau muhimu sana wakati wote katika utekelezaji wa kazi za habari kwa maeneo haya huku akiwataka kuendelea na utamaduni huo kwa maslahi mapana ya wananchi.


Kwa upande wake Meneja wa Jambo FM Redio Nickson George ameushukuru uongozi wa mkoa kwa kukubali kushiriki zoezi la ufunguzi wa kituo cha Radio na kupanda miti ikiwa nisehemu ya kuhamasisha utunzaji wa mazingira mkoani humo.

Jambo FM na Jambo Food Product leo wamefanya ufunguzi wa kituo cha Redio ambapo pamoja na mambo mengine pia wamefanya tamasha kubwa la burudani katika viwanja vya SHY COM tukio ambalo limejumuisha wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya, ngoma za asili na michezo mbalimbali ijulikanayo kama SIKUKUU JAMUKAYA kauli mbiu "Tunakula Bata la Mafanikio























Kikundi cha Msanii Mama Ushauri kkitoa burudani wakati wa Sikukuu ya JAMUKAYA katika viwanja vya Shy Com baada ya zoezi la kupanda miti.



Msanii Mama Ushauri akitoa burudani wakati wa Sikukuu ya JAMUKAYA katika viwanja vya Shy Com Mjini Shinyanga

Post a Comment

0 Comments