6/recent/ticker-posts

TAMASHA LA JUNIOR JUMBO CRDB LAFANA ,RC MNDEME AWAASA WAZAZI NA WALEZI KUFUNGULIA WATOTO WAO ACCOUNT.



Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza na watoto.


Na Mwandishi wetu - AMOS blog

Benki ya CRDB imeadhimisha siku ya Mtoto Afrika kwa  kuendesha Tamasha la Junior Jumbo kwa ajili ya utoaji elimu wa masuala ya fedha kwa watoto, wazazi na walezi sambamba na elimu ya bidhaa na huduma za benki ya CRDB ambapo watoto wamejumuika kufurahi na kujifunza masuala ya elimu ya fedha.


Tamasha la Junior Jumbo lililoandaliwa na Benki ya CRDB limefanyika leo Jumamosi Juni 17,2023 katika Viwanja yya Shule ya KOM Mjini Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme

Akizungumza wakati wa Tamasha hilo, Mndeme ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuandaa tamasha hilo akisema kuwa ni kweli ni Benki inayosikiliza na kujali wateja wake wa kira rika na kwamba baada ya tamasha hilokutakuwa na mabadiliko makubwa kwa kujenga uelewa ambao utawawezesha kuchangamkia fursa zilizopo ndani ya Benki ya CRDB.


“ Niwapongeze Benki ya CRDB kwa kuendelea kuwa wabunifu na kupelekea kuja na wazo hili la kutoa elimu ya masuala ya fedha hasa kwa watoto kwani sote tunatambua kuwa hawa ndio Taifa la kesho na wahenga wanasema “Samaki Mkunje, Angali mbichi. Benki yetu ya Kizalendo ya CRDB imekua ikifanya jitihada kubwa katika kuimarisha ustawi wa jamii yetu”,amesema Mhe. Mndeme

Amesema ni ukweli ulio wazi kuwa elimu ya fedha ina mchango mkubwa sana katika ukuaji na maendeleo ya uchumi, kujenga uchumi jumuishi, na kupunguza viwango vya umasikini ndiyo maana Serikali kote duniani zimekuwa zikitilia mkazo suala la utoaji wa elimu ya fedha (financial literacy) kwa wananchi.

“Hapa nchini, Serikali, imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za kisera ili kuongeza kasi ya utoaji wa elimu ya fedha na kukuza ujumuishi wa kifedha kwa wananchi. Sera na Mifumo hii yote imeweka mkazo mkubwa katika masuala ya elimu ya fedha ikitambua umuhmu wake katika kujenga ustawi, wa mtu mmoja mmoja na hata wa jamii kwa ujumla”,amesema Mndeme.

“Tunambua kuwa ili kufikia malengo tuliyojiwekea kama taifa katika Dira ya Maendeleo, inatuhitaji kuwajengea watu wetu uwezo hasa wa elimu ya fedha ili waweze kutambua fursa zilizopo na kushiriki kikamilifu, lakini vilevile tunaamini kuwa ili kufanikiwa katika hili ni lazima tuanzie chini kwa kuanza kuwapa watoto wetu elimu juu ya fedha na kuwajengea tabia ya kujiwekea akiba”,ameongeza Mndeme.

Amesema ili kujenga Taifa lililo imara kiuchumi, ni vyema kuanza kwa kuwekeza katika kuwapatia watoto wetu elimu ya fedha, kwani elimu ya fedha ndiyo inaleta msukumo mkubwa katika kufikia malengo ya kiuchumi.


“Elimu ya fedha huathiri tabia ya kifedha kwasababu mara nyingi inakuwa ni msukumo kutoka ndani, ambao humchochea mtu kufanya maamuzi kulingana na yeye anavyofahamu. Hii inamaanisha watu wasio na msingi imara na ambao wamekuwa na uelewa mdogo juu ya masuala ya fedha wamekuwa wakipata athari hasi kwa maana ya kufanya maamuzi ya kifedha yasiyo na manufaa au muda mwengine kutofanya maamuzi kabisa kutokana na kukosa uelewa”,ameeleza Mkuu huyo wa Mkoa.


Amesema Elimu ya fedha inawapa watoto stadi muhimu za maisha ambazo zitawasaidia katika maisha yao yote kwa kuwajengea uwajibikaji wa kifedha, kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba, na kuwaweka katika njia sahihi ya maendeleo binafsi kufikia uhuru wa Kifedha (financial freedom).

“Lakini nimefurahishwa zaidi kuona malengo ya akaunti ya Junior Jumbo yameunganishwa na kufanikisha ndoto za wototo wetu katika elimu. Upo usemi unaosema urithi bora kwa mtoto ni elimu, leo naomba niongezee hapa kwa kusema kuwa “Urithi bora una jumlisha kuweka misingi bora ambayo itasaidia mtoto kupata elimu na mahitaji yake ya msingi kwa uhakika”,amesema


“Hivyo niwapongeze sana Benki ya CRDB kwa kulitambua hili na kuwawezesha wazazi kufanikisha ndoto za watoto wao katika elimu Akaunti hii ya Junior Jumbo (JJ) kwa kuwawezesha kuweka Akiba kidogo kidogo ili kufikia lengo. Niwapongeze pia kwa hamasa ambayo mmekuwa mkiitoa kwa wazazi kupitia kampeni mbalimbali ikiwamo hii ya “Timiza Ndoto yake na Junior Jumbo” ambayo pia inatoa fursa ya wazazi kujishindia ada kwa ajili ya waoto. Huu ni ubunifu mkubwa ambao unapaswa kupongezwa”,ameongeza.

Ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya sita imekuwa ikiweka mazingira wezeshi katika sekta ya kuhakikisha watoto wote wanapata elimu kupitia sera ya ‘elimu bure’, lakini mahitaji ya kuhakikisha mtoto anapata elimu bora yanajumuisha vitu vingi ambavyo pia ina mhitaji mzazi kujipanga kifedha. Hivyo basi hii ni fursa nzuri sana ambayo inapaswa kila mzazi au mlezi kuitumia.

Mkuu huyo wa mkoa pia amewasihi Wazazi na Walezi kuweka mikakati madhubuti ya kuweka akiba kwa ajili ya watoto kwani kwa kufanya hivyo wataweza kutimiza majukumu yao kama wazazi kwa maana ya kumudu mahitaji ya watoto pamoja na kuwawezesha kufikia malengo waliyojiwekea ili kujenga Taifa bora zaidi siku za usoni.


Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Kanda ya Magharib Benki ya CRDB, Jumanne Wagana Benki ya CRDB inachukulia kwa umuhimu mkubwa suala la kuwatengenezea mazingira yaliyo bora watoto wetu, kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kuwawezesha kutimiza malengo yao pamoja na kuandaa taifa lililo imara hapo baadae.


Mkurugenzi wa shule za KOM Jackton Koy akizungumza kwenye maadhimisho hayo.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga akizungumza wakati wa maadhimisho hayo.


Mkuu wa mkoa wa Shinyanga akizungumza na meneja wa CRDB .








Mkurugenzi wa shule ya Hilbat Dkt Clement akizungumza kwa niaba ya wakurugenzi shule za binafsi.


Mwakilishi wa wazazi Alfred Kailembo akizungumza kwaniaba ya wazazi.


Kaimu meneja wa benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Jumanne Wagana akizungumza kwenye Maadhimisho hayo.

Post a Comment

0 Comments