6/recent/ticker-posts

WDC KATA YA SHINYANGA MJINI YARIDHISHWA MIRADI KABAMBE ILIYOANZISHWA..WAHUZUNIKA SATURA KUPELEKWA DAR.






Kaimu Mtendaji wa kata ya Mjini Mathias Salu akisoma taarifa ya mradi wa bustani ya kupumzikia

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Kamati ya Maendeleo ya Kata (WDC) ya Mjini Manispaa ya Shinyanga ikiongozwa na Diwani wa kata hiyo Mhe. Gulam Hafeez Mukadam imetembelea miradi inayotekelezwa katika kata ya Mjini ikiwemo ujenzi wa Bustani za kupumzikia, Maegesho ya Pikipiki na Bajaji , Stendi ya Hiace, Soko Kuu, Soko la Wajasiamali, mitaro na madarasa na vyoo katika shule ya Awali na Msingi Mwenge.


Ziara hiyo imefanyika leo Jumatano Juni 7,2023 ambapo Wajumbe wa kamati ya WDC Kata ya Mjini wameeleza kuridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye kata hiyo ambayo ndiyo inabeba muonekano wa Mji wa Shinyanga.


Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Diwani wa kata ya Mjini Mhe. Gulam Hafeez Mukadam amesema katika maeneo yote ya miradi waliyotembelea wananchi wameeleza kuridhika na kufurahia miradi ya maendeleo inayotekelezwa ambayo kwa kiasi kikubwa imefanya Manispaa ya Shinyanga kubadilika na kuwa na mandhari yanayovutia na kupendeza.



Mwalimu Mkuu wa shule ya awali na msingi Mika Kakema akisoma taarifa ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo


Diwani wa kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga Mhe. Gulam Hafeez Mukadam akitembelea shule ya awali na msingi Mwenge.


Post a Comment

0 Comments