6/recent/ticker-posts

TIMU YA UVCCM MASEKELO YAONDOLEWA KIBABE NA TIMU YA UVCCM NGOKOLO KATIKA MASHINDANO YA DKT. SAMIA CUP SHINYANGA

Katika mchezo huo Timu ya UVCCM Masekelo imeshindwa kutamba mbele ya Timu ya UVCCM Ngokolo baada ya dakika tisini za mchezo kumalizika bila kufungana huku timu hiyo ikishindwa kufurukuta katika upigwaji wa mikwaju ya penart ambapo timu ya UVCCM Ngokolo imefunga penart tano kwa nne dhidi ya timu ya UVCCM Masekelo na kuifanya timu ya masekelo kuaga katika mashandano hayo huku UVCCM Ngokolo ikipata tiketi ya kwenda kushiriki katika hatua ya robo fainali.

Pia katika mchezo mwingine Timu ya Ngokolo Sekondari imekubali kuaga mashindano hayo baada ya kupokea kichpo cha magoli mawili kwa sifuri kutoka kwa Timu pinzani ya Wapigadebe kutoka kata ya Ndembezi.

Wamuzi wa mchezo wakijiandaa kwa ajili ya mpambano katika uwanja wa Shy com





Timu ya Ngokolo Sekondari ikipambana na Timu pinzani ya Wapigadebe kutoka kata ya Ndembezi katika uwanja wa kitangili.
Timu ya Wapigadebe kutoka kata ya Ndembezi ikipambana na Timu ya Ngokolo Sekondari kutoka katika kata ya Ngokolo
Timu ya Wapigadebe kutoka kata ya Ndembezi wakipanga mbbinu za kuiondoa Timu ya Ngokolo Sekondari katika Mashindano 

Post a Comment

0 Comments