Mkuu wa
mkoa wa Shinyanga Mhe.Christina Mndeme amezindua mradi wamaji wenye thamani ya
Shilingi Bilioni 1.058 unaotekelezwa na Shirika la Lifewater International kwa
kushirikiana na Wakala wamaji na Usafi wamazingira Vijijini (RUWASA)Wilaya ya
Shinyanga .
Akizungumza
kwenye uzinduzi wa mradi huo,Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Christina
Mndeme amelipongeza Shirika la Lifewater International , kwa kutekeleza mradi
wa maji ndani ya mkoa wa Shinyanga ambao umetekelezwa kwenye kata ya Mwalukwa halmashauri
ya wilaya ya Shinyanga hali itakayo saidia kuwaondolea wananchi changamoto ya
kutumia maji yasiyo kuwa safi na salama pamoja na kutembea umbali mrefu wakitafta
huduma ya maji.
Mhe.Mndeme amesema Serikali ya awamu ya Sita chini
ya uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan inasisitiza sana upatikanaji wa maji karibu na
makazi ya wananchi ili kufikia adhima ya Dkt.Samia ya kumtua mama ndoo kichwani
na kuondokana na adha ya ukosefu wa maji safi na salama, pamoja na kuugua
magonjwa yatokanayo na matumizi ya maji ambayo siyo salama kiafya.
“Tunalishukuru
sana Shirika hili la Lifewater International kwa kutekeleza mradi huu wa maji Ndani
ya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga , ambapo tunaomba mradi huu pia ufike
na kwenye maeneo mengine ambayo yana shida ya maji safi na salama,”amesema Mndeme.
Naye
Mkurugenzi wa Shirika la Lifewater International Tanzania Devocatus Kamara, amesema
mradi huo umetekelezwa kwenye kata ya Mwalukwa halmshauri ya wilaya ya
Shinyanga kwa kiasi cha Shilingi za kitanzania bilioni 1.058 huku akieleza kuwa mradi
huo unatarajia kukamilika Mwezi March mwaka 2024.
Kwa upande wao baadhi ya Wananchi wa Kata ya Mwalukwa wameishukuru serikali pamoja na Shirika la Lifewater International kwa kuwajengea mradi wa maji katika kata hiyo mradi utakao saidia kupunguza adha ya kutembea umbali mrefu wakitafta huduma ya maji na kuondokana na changamoto ya kutumia maji yasiyo kuwa safi na salama.
0 Comments