6/recent/ticker-posts

PALLANGYO BROTHERS WAMPA SHETANI KIPIGO KANISA LA EAGT ADONAI BUGWETO SHINYANGA ,MAMIA WAMKIRI YESU KRISTO KUWA MWOKOZI WA MAISHA YAO

Na Amo Blog Shinyanga

Waimbaji watatu kutoka mkoani Arusha, wanaounda kundi la Pallangyo Brothers, wenye kimo kifupi (Kibirikizi) kwa kushirikiana na Kanisa la Eagt Adonai Bugweto Manispaa ya Shinyanga, wameleta mamia msalabani katika mkutano mkubwa wa Injili wa siku nane ulio andaliwa na uongozi wakanisa la Eagt Adonai Bugweto.

Mkutano huo uliofanyika katika viwanja vya Kanisa hilo, huku Mhubiri wa mkutano huo akiwa mchungaji Alexander Ndambo kutoka mkoani Dodoma umekusanya mamia ya wakazi wa Manispaa ya Shinyanga waliokuwa wakisumbuliwa na changamoto mbalimbali wakihitaji kupata uponyaji kupitia mkutano hio.

 Akihubiri katika mkutano huo, Mchungaji Ndambo amebainisha kuwa, mwanadamu yoyote akimwamini Mungu ni wazi kuwa hakuna jambo lolote linaloweza kushindikana, huku akielezea kuwa dhambi ndiyo inayomtenganisha mwanadamu na Muumba wake.

Mtumishi huyo ameweka wazi juu ya hilo akisema: “Hata leo Yesu yu hai na anaweza kumpa mtu mahitaji yake wakati wowote amesema Ndambo.”

 Mchungaji Ndambo , akiwa na Mchungaji mwenyeji wa kanisa la Eagt Adonai Bugweto Mchungaji Samaytu ameeleza kuwa , hata yale ambayo watu wameyakatia tamaa, Bwana anaweza kuleta ukombozi na kumuaibisha shetani.

 Katika mkutano huo, Pallangyo Brothers wameonyesha kuwa na mguso wa pekee kwa jamii, huku watu wakijiuliza namna maumbo yao yalivyo, lakini wanaweza kumnyang’anya shetani mateka.

 Katika mkutano huo watu zaidi ya 100 wameokolewa, wengine wamefunguliwa katika vifungo vya magonjwa na maonezi ya pepo wabaya.

 Pia mchungaji Ndambo kwa kushirikiana na mchungaji Samaytu na wachungaji waliohudhuria mkutano huo, wamefanya maombi ya kuliombea Taifa la Tanzania.








































Post a Comment

0 Comments