6/recent/ticker-posts

U.W.T WILAYA YA SHINYANGA VIJIJINI WA PELEKA FURAHA KITUO CHA WAZEE BUSANDA NA WODI YA WAZAZI ZAHANATI YA USANDA

Mgeni rasmi ambaye pia ni mjumbe wa Baraza kuu UWT Taifa Ndugu Christina Gule akiwa na viongozi wa UWT wakati wa kukabidhi zawadi mbalimbali katika kituo cha kulelea wazee Busanda

Na Amo Blog Shinyanga

Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) U.W.T  Wilaya ya Shinyanga vijijini wameadhimisha wiki ya UWT katika kata Ya Usanda,kwa kutembelea kituo cha kulelea wazee cha Busanda kilichopo katika Kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na kutoa zawadi za vitu mbalimbali katika kituo hicho pamoja na kufanya usafi katika Zahanati ya Usanda na kuwapatia mahitaji muhimu  kinanama waliojufungua katika wodi ya wazazi iliyopo katika Zahanati hiyo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya wiki ya UWT.

Umoja wa Wanawake wa CCM U.W.T  Wilaya ya Shinyanga vijijini wametoa msaada huo jana Okitoba 28,2023 walipotembelea katika kituo cha kulelea wazee cha Busanda kilichopo katika Kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya wilaya hiyo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya wiki ya U.W.T , ambapo Wilaya ya Shinyanga Mjini imeadhimisha kwa kushiriki katika shughuli mbali mbali za kijamii ikiwemo kufanya usafi katika Zahanati ya Usanda na kutoa mahitaji muhimu kwa wakinamama waliojifungua katika zahanati hiyo.

Baada ya kutoa zawadi za vitu mbalimbali katika kituo cha kulelea wazee Busanda na kufanya usafi na kukabidhi zawadi kwa wakinamama walio jifungua pia wamefanya mkutano wa hadhara katika kata ya Usanda na kuwahamasisha wanawake kuwania nafasi za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa pamoja na kutoa elimu ya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wananchi.Mgeni rasmi ambaye pia ni mjumbe wa Baraza kuu UWT Taifa Ndugu Christina Gule akiwa na viongozi wa UWT wakati wa kukabidhi zawadi mbalimbali katika kituo cha kulelea wazee Busanda

Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga Vijijini Mektrida Mkali   akikabidhi  Zawadi katika kituo cha kulelea wazee Busanda 
Viongozi wa UWT wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhi zawadi mbalimbali katika kituo cha kulelea wazee Busanda
Viongozi wa UWT wakiwa kwenye mkutano wa hadhara Usanda.







Post a Comment

0 Comments