6/recent/ticker-posts

MCHIMBAJI MDOGO WA MADINI SHINYANGA AIBUKA KIDEDEA UCHAGUZI WA MWENYEKITI WA JUMUIA YA WAZAZI SHINYANGA

Mchimbaji mdogo wa madini Fadhili Salmon Nyavyuma baada ya kuchaguliwa kwa kishindo kuwa mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga Vijijini.

Na Amo Blog Shinyanga.

Mchimbaji mdogo wa madini Fadhili Salmon Nyavyuma kutoka kata ya Mwakitolyo Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini amechahuliwa na wajumbe wa mkutano mkuu maalumu kuwa mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga Vijijini

Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa ofisi ya Chama Chamapinduzi mkoa wa Shinyanga (NSSF) kufatia aliyekuwa mwenyekiti wa jumuiya hiyo Marehemu Hamis Shikuba kufariki duni mwezi Mei ,22,2023 hali iliyo pelekea wilaya hiyo kubaki bila kuwa na mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi kwa kipindi cha Zaidi ya miezi mine.

Akitangaza matokeo hayo msimamizi mkuu wa uchaguzi Bandora Salumu Mirambo ambaye ni Katibu wa Elimu , Malezi na Mazingira Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga amemtangaza Fadhili Salmon Nyavyuma kuwa mshindi wa uchaguzi huo kwa kupata kula 360 kati ya kura 398 zilizo pigwa na kuwashinda washindani wake Angelina Maganga aliyepata kura 3 na Pastory Simion aliyepata kura 27.

Aidha Bandora Salmu ambaye ni Katibu wa Elimu , Malezi na Mazingira Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa amesema kuwa kati ya kura 398 kura 390 ni kura harali na kura zilizo haribika na kura 8 ambapo amewashukuru wapigakura kwa kutimiza haki yao yamsingi kwa kumchagua kiongozi atakaye waletea maendeleo katika jumuiya ya wazazi na chama cha mapinduzi kwa ujumla.

Akitoa Shukrani baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga vijijini Fadhili Salumoni Nyavyuma amewashukuru wajumbe kwakumchagua kuwa mwenyekiti wa jumuiya hiyo huku akiahidi kuimarisha jumuiya hiyo kwa kuanzisha mradi wambuzi kila kata ili mbuzi hao watakapo zaa waweze kusambazwa kwenye matawi ikiwa nisehemu ya kuimarisha uchumi wa jumuiaya hiyo.

Pia Nyavyuma ameahidi kufanya ziara ya kutembelea kata na matawi yote iliwaweze kujadiliana namna ya kuchochea maendeleo ya jumuiya ya wazazi na chama cha mapinduzi kwa ujumla.

Msimamizi mkuu wa uchaguzi Wa mwenyekiti jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga vijijini Bandora Salum ambaye ni Katibu wa Elimu , Malezi na Mazingira Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa akitangaza matokeo ya uchaguzi.

Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wa mwenyekiti jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga vijijini .Msimamizi mkuu wa uchaguzi Wa mwenyekiti jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga vijijini Bandora Salum akiwa na mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi wilaya ya Shinyanga Vijijini Edward Ngelela.Mchimbaji mdogo wa madini Fadhili Salmon Nyavyuma baada ya kuchaguliwa kwa kishindo kuwa mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga Vijijini.

Katibu Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga vijijini Erenestina Richard kitoa utaratibu wa uchaguzi kwa wajumbe .
Awali wagombea nafasi ya Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga Vijijini wakiwa wameketi pamoja wakisubiri kuomba kura kwa wajumbe.
Awali wagombea nafasi ya Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga Vijijini wakiwa wamesimama kwa pamoja wakisubiri kuomba kura kwa wajumbe.
Katibu jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga vijijini Ashura Ngade akitoa utaratibu wa uchaguzi kwa wajumbe .
Katibu jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga vijijini Ashura Ngade akitoa utaratibu wa uchaguzi kwa wajumbe 
Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wa mwenyekiti jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga vijijini .
Mchimbaji mdogo wa madini Fadhili Salmon Nyavyuma akiomba kura kwa wajumbe nafasi ya kuwa mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga Vijijini.
Awali wagombea nafasi ya Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga Vijijini wakiwa wamekaa kwa pamoja wakisubiri kuomba kura kwa wajumbe.
Wajumbe kutoka jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga Vijijini wakisubiri kusikiliza sera za wagombea kabla ya uchaguzi.
Wajumbe kutoka jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga Vijijini wakisubiri kusikiliza sera za wagombea kabla ya uchaguzi.
Katibu Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga vijijini Erenestina Richard kitoa utaratibu wa uchaguzi kwa wajumbe .
















Mchimbaji mdogo wa madini Fadhili Salmon Nyavyuma akiomba kura kwa wajumbe nafasi ya kuwa mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga Vijijini.
Mchimbaji mdogo wa madini Fadhili Salmon Nyavyuma akiomba kura kwa wajumbe nafasi ya kuwa mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga Vijijini.
Mchimbaji mdogo wa madini Fadhili Salmon Nyavyuma akiomba kura kwa wajumbe nafasi ya kuwa mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga Vijijini.



Wajumbe wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga Vijijini wakijiandaa kupiga kura


Zoezi la kuhesabu kura likiwa linaendelea .

Post a Comment

0 Comments