Mkuu
wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akikabidhi mahindi kwa waanga
walioezuliwa makazi yao na mvua katika kata ya Chibe.
Na Amo Blog Shinyanga
Mkuu wa
Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi amegawa blangeti na Mahindi kwa waanga
ambao makazi yao yaliezuliwa na upepo kutoka na mvua kubwa iliyonyesha Tarehe Okitoba
17,2023 ambapo jumla ya Kaya 8 ziliathrika na mvua hiyo ikiwemo kukosa makazi
ya kuishi.
Akikabidhi msaada
huo katika Ofisi ya Mtendaji wa kata ya Chibe Mhe. Samizi ametoa pole kwa
waanga wote walio kumbwa na tatizo hilo huku akiwataka wakazi wakata hiyo
kujenga nyumba imara ili kuepuka changamoto zinazo jitokeza kutokana na mvua
kubwa zinazo endelea kunyesha.
"Poleni
sana ndugu zangu kwa maafa yaliyowapata Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan anawajali na anawatambua ndo maana leo nipo hapa
kwa ajili ya kuwapatia blangeti kwa ajili ya kujikinga na baridi pamoja na
mahindi ya chakula lakini pia niwatake
msimu wa mvua utakapopita tuboreshe nyumba zetu na tujenge nyumba zenye
uimara" amesema Mhe. Samizi
Pia Mhe.
Samizi amegawa jumla ya blangeti 40 katika kaya 8 zenye watu 40 pamoja na
mahindi tani 1 kwa watu 40.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akikabidhi Blangeti kwa waanga walioezuliwa makazi yao na mvua katika kata ya Chibe. Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akikabidhi mahindi kwa waanga walioezuliwa makazi yao na mvua katika kata ya Chibe. Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akikabidhi blangeti kwa waanga walioezuliwa makazi yao na mvua katika kata ya Chibe.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akikabidhi mahindi kwa waanga walioezuliwa makazi yao na mvua katika kata ya Chibe. Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akikabidhi mahindi kwa waanga walioezuliwa makazi yao na mvua katika kata ya Chibe. Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akikabidhi blanketi kwa waanga walioezuliwa makazi yao na mvua katika kata ya Chibe. Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akikabidhi blangeti kwa waanga walioezuliwa makazi yao na mvua katika kata ya Chibe.
0 Comments