Na Kareny Masasy, Kishapu
UMOJA wa wanawake
Tanzania wa chama cha Mapinduzi (UWT) mkoa wa Shinyanga umeeleza
ukatili uliokuwa unapatikana kwa wanawake sababu ya ukosefu wa maji safi
na salama Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzaia Samia Suluhu ameuondoa
ukatili huo.
Hayo yamesemwa leo tarehe
29,Novemba,2023 na wajumbe wa UWT mkoa
wakiongozwa na mbunge viti maalum Santiel Chilumba
ambapo amesema wakala wa maji safi na mazingira vijijini
(Ruwasa) mkoa wa Shinyanga wamefanya kazi kubwa ya kutekeleza miradi
ambayo serikali imetoa fedha nyingi.
Chilumba amesema kero
kubwa ilikuwa ni maji na kipindi cha miaka miwili ya Rais Samia Suluhu ametoa
fedha nyingi kwenye miradi ya maji lengo kuondoa kero hiyo kwa wananchi na
waisimamie vizuri kwani miradi inatakiwa kuwa endelevu.
“Mradi huu ni mkubwa kwa
mkoa mzima wa Shinyanga kwa kutumia fedha nyingi na hatutaki Rais
akwamishwe ila tunaipongeza Ruwasa ndani ya mkoa huu haijamkwamisha Rais ipo
bega kwa bega”alisema Chilumba.
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa
Shinyanga Grace Bizuru amesema kitu ambacho wamejivunia
nikuona wanawake hawateseki tena na utafutaji wa maji hali ambayo ilikuwa
ikiwafanya wapate changamoto ndani ya ndoa zao na wengine kufanyiwa vitendo vya
ukatili.
Katibu wa UWT mkoa wa
Shinyanga Aisha Kitandala amesema lengo la chama kuona
wanawake wanatatuliwa kero zao hasa upande wa maji ambao ulikuwa ukionekana
ukosefu wa maji ni chanzo cha ukatili kwa wanawake nakuwashauri
Ruwasa kutumia vibarua wanatoka kwenye eneo hilo ili wanufaike.
Mbunge wa jimbo la Kishapu
Boniface Butondo amesema ilani ya chama cha Mapinduzi
waliyokuwa wakiinadi imetekelezwa vizuri kwa kumtua mama ndoo kichwani kwa
vijiji hivyo kwani kilio kikubwa kwa wananchi wa vijiji hivyo
ilikuwa ni kupata huduma ya maji.
Meneja wa Ruwasa wilaya
ya Kishapu mhandisi Dicksoni Kamazima amesema ujenzi wa mradi wa
maji ya bomba katika kijiji cha Seseko hadi Ngundangali unagharimu
zaidi ya sh Bilioni 2.8 unatekelezwa na mkandarasi M/S
na Otonde Costruction and General Supplier Ltd kwa mkataba wa mwaka
mmoja.
“Mpaka sasa
tanki la maji linautekelezaji wa asilimia 88.5 na linaujazo wa lita laki
moja katika mnara wa mita 15 na kujenga vituo vya kuchotea maji 31 katika
mradi huo”amesema Kamazima.
Wakati huo huo mhandisi
Kamazima amesema wakazi 49,965 kutoka vijiji 13 vya kata tatu
vya halmashauri ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga
watanufaika na mradi wa maji wa ziwa victoria uliogharimu
zaidi ya sh Bilioni 6.6.
Mhandisi Kamazima amesema
mradi huo unatekelezwa kwa fedha za serikali na mkandarasi amelipwa
malipo ya awali huku akivitaja vijiji vitakavyo nufaika
kuwa ni Igaga A na B, Isagala, Mwamashele, Busongo, Mwamanota,
Bubinza, Lwagalalo, Mwamadulu,Nyawa,Beledi,,Lagana na Mihama.
“Utakapokamilika mradi
huo utawapunguzia muda wa kufuata maji umbali mrefu na kuwaongezea muda
wa kushiriki shughuli za kiuchumi na kijamii pia kupunguza mlipuko wa magonjwa
yatokanayo na kutumia maji yasiyo safi na salama.”amesema Kamazima.
Meneja Ruwasa mkoa wa Shinyanga
mhandisi Juliette Payovela amesema miradi hiyo ikikamilika itaweza
kuwaondolea kero wananchi kwani serikali imeleta fedha za utekelezaji na
wakandarasi wapo kazini
Diwani wa kata ya Lagana Luhende Sana amesema kata yake ina vijiji vitano ambavyo vyote vitanufaika kwani awali walikuwa wakinunua maji ndoo moja sh 1000 au kufuata umbali wa kilomita tano mto tungu.Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kishapu Rahel Madundo akitoa pongezi zakwe kwa Ruwasa
Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Shinyanga Santiel Kilumba akimpongeza meneja wa Ruwasa Shinyanga kwa kusimamia zoezi la usambazaji wa maji vijijini Mhandisi Dickson kamazima akitoa maelezo mbele ya viongozi waliotembelea miradi ya maji.
Mhandisi Dickson kamazima akitoa maelezo mbele ya viongozi waliotembelea miradi ya maji.
0 Comments