6/recent/ticker-posts

JAJI MAHIMBALI AREJESHA MATUMAINI KWA WALIO KATA TAMAA SHINYANGA ,WAZEE WAANGUA VICHEKO

Jaji mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Shinyanga Mhe.Jaji Frank Habibu Mahimbali

Na Amo Blog Shinyanga

Jaji mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Shinyanga Mhe.Jaji Frank Habibu Mahimbali,amefika katika viwanja vya zimamoto Nguzo nane halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na kusikiliza changamoto za mtu mmoja mmoja hali iliyo wafanya baadhi ya wananchi walio fika katika uwanja huo kurejesha furaha iliyo kuwa imepotea kutokana na kuwaza namna ya kupata mwafaka wa kutatua changamoto zao.

 Mhe.Mahimbali amewasikiliza wananchi hao leo Januari 24,2024 katika viwanja vya zimamoto mjini Shinyanga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya sheria nchini, ambayo kwa Kanda ya Shinyanga yatazinduliwa katika uwanja wa Zimamoto Nguzonane mjini Shinyanga Januari 27 mwaka huu katika viwanja hivyo.

Kwa upande wake Yohana Shija ambaye amefika katika viwanja hivyo akihitaji kupata msaada wakisheria amempongeza jaji Mahimbali kwa kuamua kutoka ofisini na kuwafata wananchi kisha kuwapa elimu wananchi juu ya maswalambalimbali ya Sheria huku akiomba viongozi wengine kuiga mfano huo.
Jaji mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Shinyanga Mhe.Jaji Frank Habibu Mahimbali,akitoa elimu kwa Yohana Shija aliyefika  katika viwanja vya zimamoto kwa ajili ya kupata ufumbuzi wa changamoto zinazo mkabili.

Jaji mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Shinyanga Mhe.Jaji Frank Habibu Mahimbali,akimsikiliza Yohana Shija aliyefika  katika viwanja vya zimamoto kwa ajili ya kupata ufumbuzi wa changamoto zinazo mkabili.
Jaji mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Shinyanga Mhe.Jaji Frank Habibu Mahimbali,akimsikiliza Yohana Shija aliyefika  katika viwanja vya zimamoto kwa ajili ya kupata ufumbuzi wa changamoto zinazo mkabili.

Post a Comment

0 Comments