6/recent/ticker-posts

LUHENDE JOHN FOUNDATION YATOA MSAADA KWA WANAFUNZI WALIOUNGULIWA BWENI IGUNGA

Jitihada  za wadau wa elimu zinaendelea kuonekana hii ni kutokama na  ajali ya kuungua moto kwa bweni la wanafunzi wa shule ya Sekondari Ziba iliyopo wilayani Igunga mkoani Tabora na kupelekea kuteketea kwa vitu vya wanafunzi wapatao 200 wanaosoma katika shule hiyo .

Tukio hilo lilitokea Januari 23, 2024 katika shule ya Sekondari Ziba iliyopo wilayani humo na kusababisha kuungua kwa moja ya bweni la wanafunzi wa Shule hiyo.

Awali akieleza namna tukio lilivyotokea Makamu Mkuu wa shule ya Sekondari Ziba Cassian Mbele amesema siku ya tukio hawakufanikiwa kuokoa chochote kutoka ndani ya bweni lililokuwa likiwaka moto.

"Tulipatwa na tukio la ajali ya kunguliwa na moja ya bweni la wavulana januari 23, 2024 majira ya saa 2 asubuhi ambapo wanafunzi wote walikuwa darasani, jambo la kumshukuru mungu hakuna mwanafunzi yoyote aliyedhurika zaidi ya uharibifu na wa vifaa vya wanafunzi na jengo" Amesema Mbele.

Kufatia Tukio hilo Uongozi wa shirika la Luhende John Foundation umetoa msaada wa masanduku kwa wanafunzi ambao vifaa vyao viliteketea kwamoto lengo ikiwa ni kuwasaidia wanafunzi kuhifadhi vifaa waliyopewa na wadau wa Elimu. 

Kwa upande wao wanafunzi waliokumbwa na janga hilo wameeleza namna hali ilivyokuwa baada ya tukio hilo na namna ajali hiyo alivyoathiri masomo yao huku wakilishukuru shirika la Luhende John Foundation kwa msaada wa masanduku ambayo yatawasaidia kuhifadhia misaada  waliyopewa na wadau wa Elimu. 

"Baada ya tukio hilo wanafunzi wote ilitubidi tuhamie kulala darasani kwa muda wa siku tatu na baadae tulihamishwa na kupelekwa kwenye bwalo la chakula ndipo tunapoishi mpaka sasa",.wamesema wanafunzi

"Tukio hilo lilitokea tulikuwa darasani nguo zetu zote, vitabu, Madaftari vyote viliungua kwa moto ". Wameeleza wanafunzi. 

Zoezi la utowaji wa misaada hiyo kwa waathilika wa tukio limeambatana pamoja na uzinduzi wa shirika la Luhende John foundation lenye makao makuu Mkoani Tabora ambapo katibu wa shirika hilo Abubakary Bukuku ameainisha malengo makuu ya shirika hilo kwa ni kusaidia jamii katika Nyanja ya Elimu, Michezo, Afya, uchumi pamoja na mazingira.


"Shirika la Luhende John foundation ni shirika lililoanzishwa mathubuti kwa ajili ya kusaidia wahitaji zaidi haswa katika nyanja ya Afya, Elimi, Michezo,, Uchimi pamoja na Mazingira kwa ngazi ya wilaya na Taifa kwa ujumla" Amesema Bukuku. 

Awali akizindua shirika hilo lenye makao makuu wilaya ya Nzega  katika Mkoa wa Tabora mwakilishi wa Mkuu wa wilaya hiyo afisa Tarafa Nyasa Komanya amelitaka shirika kufanya kwa kuzingatia Sheria ,kanuni na taratibu za nchi.

"Taasisi hii imeahidi kushirikiana na serikali hivyo ni matumaini yangu taasisi hii itasaidia jamii yetu, hatutakuwa tayari kushirikiana na taasisi ambazo hazifuati taratibu na sheria za nchi" Amesema Komanya. 

Hafla ya uzinduzi wa shirika la Luhende John Foundation ukiendelea.
Mwenyekiti wa Luhende John Foundation, John Luhendeakizungumza wakati wa uzinduzi wa shirika hilo.

Mwenyekiti wa Luhende John Foundation akikabidhi Sanduku kwa mwakilishi wa wanafunzi pamoja na waalimi shule ya sekondari Ziba.


Hafla ya uzinduzi wa shirika la Luhende John Foundation ukiendelea.

Hafla ya uzinduzi wa shirika la Luhende John Foundation ukiendelea.

Hafla ya uzinduzi wa shirika la Luhende John Foundation ukiendelea.

Hafla ya uzinduzi wa shirika la Luhende John Foundation ukiendelea.

Picha ya pamoja.

Post a Comment

0 Comments