6/recent/ticker-posts

KAMANDA MAGOMI AONGOZA ASKARI POLISI UPANDAJI MITI SHINYANGA,IKIWA NI SEHEMU YA JESHI LA POLISI KUTUNZA MAZINGIRA

 

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akipanda mti.

Na Amo Blog Shinyanga 

JESHI la Polisi mkoani Shinyanga, limepanda miti katika maeneo ya  Kambi na maeneo ya makazi ya Askari polisi wa  Jeshi hilo , ili kuboresha mazingira pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Zoezi hilo la upandaji miti limefanyika leo Febuari 14, 2024 na kupandwa miti 1600, katika maeneo ya kambi ya Jeshi la Polisi (FFU) na eneo la makazi ya Askari polisi uwanja wa polisi Kambarage .


Akizungumza wakati wa kupanda miti, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amesema Jeshi hilo linaunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kampeni ya upandaji miti ili kuboresha mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

“Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga tumepanda Miti 1600, lengo ni kuunga mkono juhudi za viongozi wetu katika kampeni ya upandaji miti kuboresha mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi,”amesema Magomi.

“Katika kampeni ya upandaji miti tunataka Shinyanga iwe ya kijani, na miti ambayo tunaipanda tunataka ilindwe na ikue, ,”ameongeza Magomi.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akimwagilia mti wake baada ya kupanda mti
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akipanda mti

Askari Polisi mkoa wa  Shinyanga wakionyesha utayari wakupanda miti katika maeneo ya makazi yao
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akimfundisha uzalendo mtoto juu ya utunzaji wa mazingira
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akiongoza zoezi la upandaji miti
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akimfundisha uzalendo mtoto juu ya utunzaji wa mazingira

Post a Comment

0 Comments