Mhe.Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Sinyanga Dkt Cristina Mnzava akiwa kwenye ziara ya kikazi katika Kata ya Lubaga.
Mbunge
wa viti maalumu Mkoa wa Sinyanga Dkt Cristina Mnzava amefanya ziara ya kikazi
ambapo ametembelea Shule za Sekondari pamoja na kukutana na makundi
ya wanawake wajasiliamali katika kata za Lubaga na Mwawaza katika Manispaa ya
Shinyanga
Akizungumza
na wanafunzi katika Shule za sekondari Lubaga na Mwawaza zilizopo
katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Dkt Mnzava amewataka Wanafunzi hao
wasichana na wavulana kuweka juhudi zaidi katika masomo ili kujiweka
katika nafasi nzuri kitaaluma na kuongeza kiwango cha ufaulu
Amewasisitiza
wanafunzi hao kuendelea kuwa waadilifu kwa Wazazi,walimu na jamii inayowaunguka
ambapo amewatahadharisha kutojihusisha na mapenzi katika umri mdogo, matumizi
ya pombe,Dawa za kulevya na kuepuka tabia na mazingira yote yenye viashiria
hatarishi vinavyokwenda kinyume na maadili ya kitanzania ikiwemo usagaji,
mapenzi na ndoa za jinsia moja,kwani itawaharibia mwelekeo wa maisha na
kuwasababishia fedheha.
Dkt
Mnzava ametoa zawadi ya Madaftari na kalamu kwa Wanafunzi wote waliopata ufaulu
wa Daraja la kwanza na la pili
Aidha
ameahidi kutoa jezi na vifaa vya michezo kwa timu za mpira wa miguu na mikono
kwa timu za wasichana na wavulana katika Shule ya sekondari ya Lubaga.
Amewaomba
Walimu kuendelea kushirikiana na Wazazi na walezi kufuatilia na kusimamia
mienendo ya Watoto kwa kuwa ni muda mrefu zaidi wamekuwa wakishinda nao.
“Walimu ongeeni na watoto
kuhusu afya ya uzazi hali itakayowasaidia kuepukana na mhemko wa rika balehe,
tunaamini shuleni ni mahali salama kwa usalama wao” amesema Mnzava
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa U.W.T Mkoa wa Shinyanga Bi Grace
Bizuru ametumia nafasi hiyo kuwahamasisha wanafunzi hao kuongeza
juhudi katika masomo ili kujiweka tayari kuingia kwenye soko huria la wasomi
ambapo wanahitajika wataalamu wa taaluma mbalimbali.
Katikataarifa
yake kwa Mbunge Dkt Mnzava,Mkuu wa Shule ya Sekondari Lubaga Mwalimu Hamisa
Boniface licha ya kueleza mafanikio mbalimbali amesema shule hiyo ambayo ni ya
kutwa ina kidato cha kwanza na cha pili na kwamba ilianza mnamo Mwaka jana 2023.
Amesema
shule hiyo ina jumla wanafunzi 254 wakiwemo wavulana 127 na wasichana
127, Walimu 11 kati yao wa kiume ni 8 na wakike 3 hakuna upungufu wa
Walimu, na kwamba shule hiyo ilijengwa kupitia fedha za mradi wa uboreshaji
Elimu Nchini (sequip)
Mwalimu
Hamisa amesema hali ya taaluma shuleni hapo ni nzuri hali ambayo Mkuu huyo wa
shule amesema inachangiwa na walimu kutoa motisha kwa wanafunzi wanaofanya
vizuri,kutoa adhabu kwa wanafunzi wanaofanya vibaya mitihani,kudhibiti utoro
unasababisha ufaulu hafifu.
Ametaja
changamoto kadhaa zinazohitaji kupata ufumbuzi kwamba ni kutokuwa na vifaa
vinavyotosheleza kwenye michezo ikiwemo jezi, hali inayopunguza hamasa ya
wanafunzi kushiriki michezo, na kutokamilika kwa baadhi ya miundombinu ya shule.
Akizungumza
kwenye ziara hiyo mjumbe wa Baraza la UWT Bi. Christina Gule amesema kuelekea
Uchaguzi wa serikali za mitaa baadaye Mwaka huu 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025
wanawake wanapaswa kushiriki kikamilifu kwa kuchangamkia fursa za
uongozi.
Katika
ziara hiyo Mbunge Dkt Chrstina Mnzava ametoa madaftari (counter book) matano na
kalamu kwa kila mmoja wa wanafunzi waliopata ufaulu wa daraja la kwanza na pili
katika mitihani yao ya Mhula ili kuwahamasisha wengine kuongeza juhudi katika
masomo,ametoa taulo za kike box kumi kwa wanafunzi wa kike,lakini jezi na vifaa
vya michezo kwa shule ya Sekondari Lubaga.
Mbunge huyo pia ametoa majiko ya gesi kumi na tano kwa Mama lishe wa kata ya Lubaga na kumi na tano mengine kwa Mama lishe wa kata ya Mwawaza lengo ni kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala na kwamba ni njia ya kudhibiti ukataji miti holela kwa ajili ya matumizi ya kuni.
Aidha
akiwa katika kata ya Mwawaza amemwongezea Mtaji wa Biashara ya mboga mboga Mama
Helena Mabula na wakati huo huo amemwezesha Mkulima wa mbogamboga Bi Julietha
kafumu fedha kwa ajili ya kununua mbegu ili kuimarisha shughuli yake hiyo.
Amewataka
Wanawake kujiunga kwenye vikundi ili waweze kupata fursa mbalimbali
zinazojitokeza ikiwemo fedha kwa ajili ya kufanya shughuli za ujasiliamali
Katika ziatra yake hiyo Mbunge wa viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Dkt Christina Mnzava alifuatana na baadhi ya viongozi wa U.W.T ngazi ya Mkoa na Wilaya
0 Comments