6/recent/ticker-posts

NMB KARIBU YAKO HAACHWI MTU NYUMA YABISHA HODI KISHAPU SHINYANGA,WANANCHI WAPONGEZA UBUNIFU WA BENKI YA NMB


                   Amojmedia Blog

Wakazi wa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga wamefurika huduma ya NMB Pesa Akaunti pamoja na huduma ya Faraja Bima katika kampeni ya Kuhamasisha Ufunguaji wa Akaunti ya NMB Pesa Akaunti Isiyo na Makato ya Mwezi inayotolewa na Benki ya NMB pamoja na Akaunti ya Faraja Bima.

Kampeni hiyo inayoendeshwa na Uongozi wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi ,NMB Wilayanya Kishapu kwa kushirikiana na Amos John (Mc Mzungu mweusi ) wameendesha kampeni ya "NMB Karibu yako haachwi mtu nyuma" iliyofanyika leo katika mnada wa Mhunze Wilayani Kishapu kwa kuwapa nafasi wananchi waliojitokeza katika mnada huo kufungua Akaunti za Shilingi 1,000/= Tu na Chap Chap Akaunti zoezi lililoenda sambamba na kuelezea faida za kuwa na bima ya faraja.

"Fursa ya kwanza inayokuja na akaunti hii ni kuwa unaingia moja kwa moja kwenye Huduma Jumuishi za Kifedha kupitia NMB, watoa huduma wametapakaa kote kuhakikisha kila Mtanzania anakuwa sehemu ya huduma hii inayokuja chini ya kaulimbiu ya ‘Haachwi Mtu".

"Kupitia NMB Pesa, utakuwa umeingia moja kwa moja katika huduma ya NMB Mkononi, inayokupa wigo mpana wa kujihudumia na kuhudumiwa kibenki bila kuja matawini ama katika ofisi za benki yetu ambako utafanya miamala na malipo na manunuzi kidigitali".

Tazama picha zote za matukio hapa chini.





























Post a Comment

0 Comments