6/recent/ticker-posts

WANACHAMA NA MASHABIKI WA TIMU YA SIMBA TAWI LA SHYBEST SHINYANGA WAJIUNGA NA NMB NA KUPATA KADI ZA UANACHAMA


Na Amoj Media

Kupitia kampeni ya (Mtaa kwa Mtaa Shabiki Tutakutambua kwa kadi) inayo endeshwa na benki ya NMB Tawi la Manonga kwa kushirikiana na mc mzungumweusi imefanikiwa kufungua Akaunti zawanachama ,Shabiki na viongozi wa Tawi la Shybest Shinyanga ,Ubaya Ubwela  na kutoa elimu ya bidhaa zinazo tolewa na benki hiyo
.
Zoezi hilo limeendeshwa na afsa masoko wa benki hiyo John Kimaro ,Albini Mpona kwa kushirikiana na mc mzungu mweusi kampeni ambayo pia imefanikiwa kupita nyumba kwa nyumba kwa ajili ya kufungua akaunti za wanachama na shabiki wa Timu ya simba katika Manispaa ya Shinyanga.

Nao baadhi ya wanachama Kindakindaki wa Timu ya Simba tawi la Shybesty wameushukuru na kuupongeza uongozi wa Benki ya Nmb kwa kuanzisha Akaunti za benki hiyo zenye Rangi ya Timu ya Simba kwa kuwa kadi hizo zitawawezesha pia wanachama kulipia ada zao kwa kutumia Akaunti hizo.
''Benki ya NMB tunasema anza  msimu mpya waligi ukiwa na kadi yako ya uanachama kupitia matawi yetu yote ya NMB

 yaliyopo karibu yako ili  #Usiachwe nyuma .(NMB Karibu yako)amesema mpona''

TAZAMA PICHA ZA MATUKI YOTE HAPA CHINI. 

Na Amoj Media Shinyanga


Post a Comment

0 Comments