6/recent/ticker-posts

HAFLA YA MWALIMU SPESHO YAFANA SHINYANGA, BENKI YA NMB MANONGA YATANGAZA NEEMA NA KUWAPA ELIMU YA MASULUHISHO YA KIFEDHA WALIMU

 

Na Amoj Media Shinyanga.

Benki ya NMB imeandaa Semina ya Mwalimu Spesho ambayo imehusisha utoaji wa mafunzo na kueleza fursa mbalimbali zanazo patikana katika benki hiyo kwa Walimu wa Kanda ya Magharibi ,Hafla iliyofanyika  Katika ukumbi wa Makindo Hall Uliyopo Manispaa ya Shinyanga mkoani humo.

Akizungumza kwenye semina hiyo,Meneja Mwandamizi Idara ya Wateja Binafsi Makao makuu Qeen Kinyamagoha amesema,walimu ni wadau  wakubwa katika biashara na kwamba wana mchango mkubwa katika Benki ya NMB.

“Tunathamini mchango wao mkubwa kwetu NMB, tumeona tuje na Masuluhisho ambayo yataenda kuwasaidia Walimu, Tunajua wanafanya shughuli mbalimbali nje ya ajira hivyo tumeona tuwawezeshe katika shughuli hizo wanazozifanya na tumeamua kuja na Mwalimu Spesho" amesema Qeen

Aidha Qeen amesisitiza kuwa semina hiyo elekezi imelenga kuboresha ustawi wa watumishi hususani walimu na kuunga Mkono juhudi za Serikali za kuboresha maisha ya watumishi kwa ujumla.

 Semina hiyo imeshirikisha walimu kutoka Halmashauri za Manispaa ya Shinyanga na Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambao wamepewa mafunzo kuhusu elimu ya fedha ,kuweka akiba, mikopo ya elimu,mikopo ya  vyombo vya moto, biashara ndogondogo, na mikopo ya kilimo na Bima.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mary Maka akizungumza kwenye mafunzo hayo ameishukuru NMB kwa kuboresha Maisha ya watumishi wakiwemo walimu.

Aidha Maka amesema kongamano hilo  lina manufaa makubwa kwa watumishi, ambao wamepewa elimu juu ya Matumizi sahihi ya fedha ,ikiwemo uhifadhi wa fedha na fursa ya mikopo mbalimbali ambayo inaendeshwa na Benki ya NMB.

 Kwa upande wao baadhi ya walimu walio patiwa mafunzo hayo kupitia hafla ya Mwalimu Spesho walimu  wamejua sehemu sahihi ya Kwenda kuchukua mikopo ambayo haitowaumiza kupitia Benki ya NMB.


TAZAMA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINIHINI.


TAZAMA PICHA CHINI HAFLA INAENDELEA











Post a Comment

0 Comments