Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Samson Hango ameongoza
sherehe za mahafali ya 16 kidato cha nne mwaka 2024 shule ya Sekondari Kom ‘
Kom Secondary’ iliyopo katika eneo la Butengwa katika manispaa ya Shinyanga
ambapo jumla ya wanafunzi 131 kati yao wasichana wavulana
wamehitimu elimu ya kidato cha nne katika shule hiyo.
Mahafali hayo yamefanyika leo Jumamosi Novemba 23,2024 katika viwanja vya shule hiyo na kuhudhuriwa na mamia ya wazazi,wageni waalikwa,wanafunzi na watu mbalimbali wenye mapenzi mema.
Akizungumza wakati wa Mahafali,Mgeni rasmi Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Samson Hango aliwataka wazazi na walezi kuhakikisha wanawalipia ada watoto wao kwa wakati.
“Nimeambiwa kuna baadhi ya wazazi wanachelewa kulipa ada.Niwakumbushe tu kuwa ukimpeleka mtoto katika shule binafsi nivizuri kuhakikisha unalipa ada,. Elimu ni gharama, hata kwenye shule za serikali ‘ Public Schools’ kuna gharama,kuna nguvu za wananchi wanachangia pia”,alisema Hango.
“Ni muhimu kumpeleka shule mtoto mara tu shule inapofunguliwa,kwani shule ikifunguliwa masomo yanaanza. Usimuweke mtoto nyumbani,anafanya nini nyumbani muda wa shule?,alihoji Hango.
Afisa Elimu huyo alitumia fursa hiyo
kuwakumbusha wazazi kuwakatia bima ya afya watoto wao ili kurahisisha matibabu
pindi wanapougua.
Hango aliipongeza shule ya Kom kwa mwenendo mzuri kitaaluma na kinidhamu kwani imeendelea kufanya vizuri katika mitihani mbalimbali ngazi na mkoa na taifa.
Naye Mkurugenzi wa shule ya Kom Sekondari Jackton Koyi ameishukuru serikali kwa ushirikiano ambao imekuwa ikiwapa katika kuhakikisha kuwa shule hiyo inafikia malengo yake.Amesema Kom sekondari tangu kuanzishwa kwake imekuwa daraja la elimu kwa wanafunzi ambao wengi wamekuwa wakiingia kidato cha tano na kujiunga katika vyuo mbalimbali.
“Naomba wazazi muendelee
kutuamini na kuleta wanafunzi katika shule hii ambayo imekuwa ikifanya vizuri
katika mitihani mbalimbali”,ameeleza Koyi.
Koyi amesema kuwa Mbali na kuwa na shule ya sekondari Kom,pia kuna shule ya awali na shule ya msingi Kom iliyoanzishwa mwaka 2016 ipo nyuma ya ofisi za KASHWASA umbali wa takribani mita 500 kutoka shule ya sekondari Kom.
Awali akisoma taarifa ya shule mkuu wa shule ya sekondari Kom Grace Mutabilwa, amesema idadi ya wanafunzi waliohitimu kidato cha nne mwaka huu ni 131.
Mgeni Rasmi ambaye ni Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Samson Hango akiwatunuku vyeti wahitimukatika sherehe za mahafali ya 16 kidato cha nne mwaka 2024 shule ya Sekondari Kom akiwa na mkurugenzi wa Shule hiyo Jackton Koyi

Mgeni Rasmi ambaye ni Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Samson Hango akizungumza na wazazi na walezi katika sherehe za mahafali ya 16 kidato cha nne mwaka 2024 shule ya Sekondari Kom akiwa na mkurugenzi wa Shule hiyo Jackton Koyi
Mkuu wa shule ya Sekondari Kom, Grace Mutabilwa akitoa taarifa ya shule wakati wa Mahafali ya 16 kidato cha nne shule ya Sekondari Kom.
Walimu wa shule ya Sekondari Kom,wakiburudika wakati wa Mahafali ya 16 kidato cha nne shule ya Sekondari Kom.
Wahitimu wa shule ya Sekondari Kom, wakiburudika wakati wa Mahafali ya 16 kidato cha nne shule ya Sekondari Kom.
Wahitimu wa kidato cha nne 2024 shule ya
Sekondari Kom wakiwa katika maandamano kuingia ukumbini wakati wa sherehe
za mahafali ya 16 kidato cha nne mwaka 2024 shule ya Sekondari Kom ‘ Kom
Secondary’ iliyopo katika eneo la Butengwa katika manispaa ya Shinyanga. Jumla
ya wanafunzi 131 wamehitimu elimu ya kidato cha nne katika shule hiyo.Wahitimu wa kidato cha nne 2024 shule ya
Sekondari Kom wakiwa katika maandamano kuingia ukumbini wakati wa sherehe
za mahafali ya 16 kidato cha nne mwaka 2024 shule ya Sekondari Kom ‘ Kom
Secondary’ iliyopo katika eneo la Butengwa katika manispaa ya Shinyanga. Jumla
ya wanafunzi 131 wamehitimu elimu ya kidato cha nne katika shule hiyo.
0 Comments