Ziara hiyo imeandaliwa na Shirika mwenyeji YAWE ili kuwapa Fursa Viongozi na Wanajumuiya ya JECA kutembelea mirada ya UFUGAJI NYUKI, Upandaji Miti, Mradi wa Lishe na Matumizi ya Nishati Mbadala inayotekelezwa na shirika la YAWE katika mkoa wa Shinyanga na Simiyu.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo iiyofanyika leo Juni 24,2025 mkoa wa Shinyanga Mwenyekiti wa JECA, Bw.Mkanga Haji, amesema Shinyanga ni miongoni mwa mikoa iliyofanikiwa kugeuza maeneo yaliyoharibika kuwa ya kijani kwa juhudi za jamii na serikali.
“Tumevutiwa sana na juhudi za jamii za hapa Shinyanga katika kurejesha misitu na matumizi ya nishati mbadala. Tunataka kujifunza zaidi ili tukarudi Zanzibar tuweze kutumia maarifa haya kwenye maeneo yetu hasa Jozani na maeneo mengine ya visiwani,” amesema Haji.
Ugeni huo umetembelea maeneo muhimu ya kimazingira kama ikiwemo Eneo la HASHI (Hifadhi za Mazingira),Hifadhi ya Misitu Mwantini pamoja na Shule ya Msingi Ndala B ambapo wamepandamiti.
Katika maeneo hayo, wameona miradi ya
upandaji miti inayopandwa na Shirika la YAWE na TFS kwa ushirikiano wa karibu
na wananchi, ufugaji wa nyuki, na elimu ya ushirikishwaji wa jamii katika
utunzaji wa mazingira.
Naye Mwanzilishi mwenza wa Shirika la YAWE, Daniel Chunga, amesema amefarijika kupokea ugeni huo kutoka Zanzibar kwani ni ishara ya uhai na uimara wa muungano wa Tanzania Bara na Zanzibar.
“Ugeni huu ni zaidi ya mafunzo – ni alama ya mshikamano wa kitaifa. Tunakaribisha fursa kama hizi ili tujenge Tanzania moja ya kijani na endelevu,” alisema Chunga.
Kwa upande wake Katibu wa JECA Aweso Shaban Rama,ametumia
fursa hiyo kuwapongeza viongozi wakuu wa nchi, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, na Rais wa
Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi, kwa kuendelea kuimarisha muungano wa
Tanzania.
“Bila muungano thabiti tusingeweza
kufanya ziara hii ya kujifunza mambo muhimu ya mazingira. Tumesafiri watu 25
kutoka Zanzibar hadi Shinyanga na kupokelewa vizuri, hii inaonyesha matunda ya
muungano,” amesema Aweso.Mwenyekiti wa,Jumuiya ya Uhifadhi wa Mazingira ya Jozani (JECA) kutoka Zanzibar akipanda mti wakati waziara yake Shule ya Msingi Ndala B.
Mwenyekiti wa,Jumuiya ya Uhifadhi wa Mazingira ya Jozani (JECA) kutoka Zanzibar akimwagilia mti wakati waziara yake Shule ya Msingi Ndala B.
Mwenyekiti wa,Jumuiya ya Uhifadhi wa Mazingira ya Jozani (JECA) kutoka Zanzibar akimwagilia mti wakati waziara yake Shule ya Msingi Ndala B.
Uongozi wa Jumuiya ya Uhifadhi wa Mazingira ya Jozani (JECA) kutoka Zanzibar ,uongozi wa Shirika la YAWE na TFS wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa waziara katika Hifadhi ya Misitu Mwantini Shinyanga.
Uongozi wa Jumuiya ya Uhifadhi wa Mazingira ya Jozani (JECA) kutoka Zanzibar ,uongozi wa Shirika la YAWE na TFS wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa waziara katika Hifadhi ya Misitu Mwantini Shinyanga.
Uongozi wa Jumuiya ya Uhifadhi wa Mazingira ya Jozani (JECA) kutoka Zanzibar ,uongozi wa Shirika la YAWE na TFS wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa waziara katika ukumbi wa ofisi ya Hifadhi ya Misitu HASHI Shinyanga.
0 Comments