Kamishina msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi akizindua kampeni ya ABIRIA PAZA SAUTI
Na Amo Blog Shinyanga.
Wananchi wametakiwa KUPAZA SAUTI kukemea na kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi juu ya madereva wanaovunja sheria za usalama Barabarani ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kwa dereva husika lengo likiwa ni kuzue ajali barabarani.
Akizungumza wakati wa Kampeni maalum ya "ABIRIA PAZA SAUTI" iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani (RSA) mkoa wa Shinyanga iliyokwenda sambamba na utoaji wa elimu kwa abiria na madereva katika kituo Kikuu cha Mabasi katika Stendi ya mkoa (Manyoni),Kamishina msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi amesema suala la usalama barabarani ni jukumu la kila Mtu.
"madereva tumeshawafundisha Sana sasa kazi inabaki kwenu abiria kusaidia kutoa taarifa juu ya madereva wanaokiuka sheria za usalama Barabarani kwani wananchi mna jukumu kubwa la kuhakikisha usalama barabarani unakuwepo,"
Na kuongeza kuwa " unapoulizwa na Askari hali ya safari ipoje jibu kama kuna tatizo Sema ili lishughulikiwe mapema kwani ukiacha kutoa taarifa ajali ikitokea na wewe unadhurika hivyo jukumu la usalama barabarani ni letu sote, "amesisitiza SACP Janeth Magomi
Pia amewataka madereva kuepukana na tabia ya kutumia Vilevi wakati wakiwa barabarani kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na inaweza kuwa chanzo cha ajali ambacho kinaweza kuzuilika
Kaimu Meneja wa LATRA Mkoa wa Shinyanga, Denis Magembe, amesisitiza umuhimu wa matumizi ya tiketi mtandao katika kupunguza udanganyifu na kurahisisha usafiri.
"LATRA inaendelea kuhakikisha kuwa bei za usafiri ziko katika usawa na zinahusiana na gharama halisi za uendeshaji wa huduma za usafiri wa barabarani. Hii itasaidia kupunguza malalamiko ya wananchi na kuimarisha usalama barabarani, lakini pia madereva mtumie mwendo unaotakiwa",ameongeza Magembe.
"LATRA inaendelea kuhakikisha kuwa bei za usafiri ziko katika usawa na zinahusiana na gharama halisi za uendeshaji wa huduma za usafiri wa barabarani. Hii itasaidia kupunguza malalamiko ya wananchi na kuimarisha usalama barabarani, lakini pia madereva mtumie mwendo unaotakiwa",ameongeza Magembe.
Kwa upande wake balozi wa Usalama Barabarani Mkoa waTabora (RSA) Zahoro Magomba amewetaka abiria kuepukana na tabia ya kusimama kwenye basi kutokana na kukosa nafasi ya kukaa.
" ukuona dereva anaendesha mwendo ambao hamuuelewe muiteni hata kondakta muambieni kwa sababu ikitokea ajali wewe ndio utakayeathirika na hii tabia ya kusimama kwenye mabasi kwa sababu limejaa sio nzuri maana ikitokea ajali bima haitakutambua wewe uliyesimama, "ameeleza Magomba
" KAMPENI YA "ABIRIA PAZA SAUTI" ni mahususi kabisa kwa ajili ya kuwakumbusha abiria kuwa wana wajibu wa kushiriki katika mapambano dhidi ya ajali za barabarani kwani dereva anavyofanya makosa abiria wakachukua jukumu la kutoa taarifa kwa Polisi na hatua zikachukuliwa basi itasaidia hata wengine kutotenda makosa, "amesema Self
0 Comments